TRA

TRA

Wednesday, June 14, 2017

Muasi Bosco Ntaganda kutoa ushahidi

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Aliyekua kiongozi wa waasi nchini Congo, Bosco Ntaganda anatarajiwa kutoa ushahidi leo katika mahakama ya kimatafa ya ICC.

Ntaganda aliyepewa jina la 'The Terminator ' atasimama kizimbani ikiwa ni takriban miaka miwili baada ya kesi kuanza.

Ntaganda anashutumiwa kutekeleza uhalifu na uhalifu dhidi ya binaadam unaodaiwa kutekelezwa na vikosi vyake.
 

 Bosco Ntaganda maarufu 'Terminator' 


Mashtaka yanasema kuwa kati ya mwaka 2002 na 2003 vikosi vyake vya uasi walivamia eneo la Ituri, wakatekeleza mauaji na vitendo vya kuwabaka raia.

Mwaka 2015, alikutwa na hatia kwa makosa 13 ya uhalifu wa kivita ikiwemo kuwasajili watoto wa umri wa chini ya miaka 15 kwenye jeshi na makosa mengine ya uhalifu dhidi ya binadamu.

Jopo lake la utetezi limepanga kuwaita mashuhuda 109 na wataalam wanne. Hii ndio sababu kesi hiyo inatarajiwa kuendelea kwa miezi kadhaa. Ikiwa atakutwa na hatia atahukumiwa kifungo cha mpaka miaka 30 gerezani.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger