
Rais
wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DARUSO)
Mhandisi John Jilili(katikati) akisisitiza jambo wakati wa mkutano na
waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano uliolenga
kupongeza juhudi za kuleta ukombozi wa kiuchumi zinazofanywa na Rais
Dkt. John Magufuli. Kulia ni Makamu wa Rais wa Serikali hiyo bi
Anastazia Anthony na kushoto ni Waziri wa michezo,Haiba na Burudani Bw.
Mabina David

Rais
wa Serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (DARUSO) Mhandisi
John Jilili akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari leo Jijini Dar es
Salaam wakati wa mkutano uliolenga kupongeza juhudi za kuleta ukombozi
wa kiuchumi zinazofanywa na Rais Dkt. John Magufuli. Kushoto ni Waziri
wa michezo,Haiba na Burudani bw. Mabina David.

Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano huo.
NA FRANK MVUNGI-MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amepongezwa kwa kazi za kizalendo
anazoendelea kuzifanya kwa maslahi mapana ya Taifa
Akizungumza na vyombo
vya habari jijini Dar es Salaam, Rais wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam (DARUSO), Mhandisi John Jeremiah amesema wanaunga mkono jinsi
suala la mchanga wa madini (makinikia) linavyoshughulikiwa na Serikali ikiwa ni
moja ya hatua za kuleta mageuzi ya kweli na kujenga Tanzania mpya.
“Tofauti na wale
wanasiasa wanaobeza juhudi za Rais Mgufuli sisi wana DARUSO tunapenda
kumuhakikishia kuwa tuko pamoja nae kifikra, kimikakati na kimaombi na
tunaamini kuwa fedha iliyopaswa kulipwa na ACACIA kwa Tanzania tangu 1998 hadi
2017 zitalipwa mara moja”Alisisitiza Jeremiah
Aliongeza kuwa ripoti
ya kamati iliyoongozwa na Profesa Michael Ossoro imebainisha kuwa fedha
zilizopotea zingeweza hudumia bajeti ya miaka mitatu hivyo juhudi za kulinda
rasilimali za Taifa zinapaswa kuungwa mkono na kila mtanzania
“DARUSO tunapenda
kukumbusha kuwa vita hii sio ya chama chochote cha siasa bali ni vita ya
watanzania wote kwa hivyo tusimame na kuungana na Mhe. Rais wetu Dkt. Magufuli
kwenye mapambano haya.” Alisisitiza Mhandisi Jeremiah
Mwandisi Jeremiah
amesema kuwa kiwango hicho cha fedha kingetosha kuhudumia huduma za kijamii
hivyo kuwapa Watanzania unafuu wa maisha.
“Tunapenda kumpongeza
Mhe. Rais kwa muelekeo mzuri wa juhudi zake za kizalendo zilizomfanya Mwenyekti
Mtendaji wa Kampuni ya (Afica) Barrick Gold Mining Professor John Thornton kuja
Tanzania kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huu”.Alisisitiza Mwandisi
Jerem
SHARE
No comments:
Post a Comment