TRA

TRA

Tuesday, June 13, 2017

Iran yafuzu kwa Kombe la Dunia 2018

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !

Mkufunzi wa Iran kwa sasa ni mkufunzi msaidizi wa zamani wa Manchester United Carlos Queiroz

Iran imekuwa nchi ya pili kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2018 baada ya kulaza Uzbekistan 2-0 mjini Tehran.

Mabao kutoka kwa Sardar Azmoun na Mehdi Taremi yalihakikisha Iran, ambayo mkufunzi wake ni Carlos Queiroz, itarejea tena kucheza Kombe la Dunia kwa kufuatiliza kwa mara ya kwanza. 

Ushindi wao uliwawezesha kufungua mwanya wa alama nane kati yao na wapinzani wao, ambao wamo nafasi ya tatu kwenye jedwali.

Mabingwa mara tano Brazil walikuwa taifa la kwanza kujiunga na wenyeji Urusi katika kufuzu kwa michuano hiyo ya mwaka ujao nchini Urusi.

Timu mbili za kwanza katika kila kundi, kati ya makundi mawili ya kufuzu katika bara Asia zitafuzu, nazo timu zitakazomaliza nafasi ya tatu kila kundi zikutane katika mechi ya muondoano ya kufuzu.

CHANZO:BBC

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger