TRA

TRA

Thursday, June 22, 2017

Manchester City yamwinda Dani Alves

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
Juventus imethibitisha kwamba itamwachilia huru beki wa kulia Dani Alves katika mwaka wa mwisho wa kandarasi yake.

Mkufunzi wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola amedaiwa kutaka kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 ambaye walijuana naye tangu akiwa mkufunzi wa Barcelona.

Akizungumza kwa vyombo vya habari vya Italy siku ya Jumatano, afisa mkuu wa klabu hiyo Beppe Marotta amesema kuwa Alvez amekuwa na hamu kucheza katika klabu nyingine.

Beki wa upande wa kulia wa Juventus Dani Alves kuelekea Manchester City 

Marotta amesema kuwa Juventus inatumai kuafikiana kuhusu kandarasi yake na Alves.Amemtakia maisha mazuri mchezaji huyo.

Alves amekuwa na Juve kwa mwaka mmoja , baada ya kushinda na Serie A mbali na kufika fainali ya kombe la vilabu bingwa Ulaya.
kabla ya kujiunga na klabu hiyo alikuwa ameichezea barcelona kwa kipindi cha miaka minane.

Misimu mitatu kati yazo ilikuwa chini ya ukufunzi wa Guardiola, kipindi ambacho wawili hao walijishindia mataji mawili ya kilabu bingwa, mbali na kombe la La Liga mara tatu.

CHANZO: BBC

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger