Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akiwa kwenye mkutano wa mameya jijini Mashad nchini Iran
|
NA MWANDISHI MAALUM, MASHAD, IRAN
MEYA
wa Jiji la Dar es salaam Isaya Mwita amekuwa gumzo katika mkutano
uliomalizika jana Jijini Mashahad Nchini Iran baada ya kusema kwamba
Tanzania haina dini ila watu wake wana dini.
Meya
ambaye yupo Nchini Iran kwa ziara ya kikazi ya siku 10, alijikuta
kwenye gumzo hilo wakati akichangia mada iliyokuwa ikiendelea ndani ya
mkutano huo ambao ulimalizika jana.
Meya
alisema kwamba Tanzania ni Nchi ya amani ambayo haijawahi kuwa na
ubaguzi wa rangi, dini wala kabila na kwamba kila mmoja aliyepo ndani ya
nchi hiyo anajivunia kuwa Mtanzania.
Alisema
hali hiyo imekuwa ni tofauti katika maeneo mengine kwani yapo
mataifa ambayo hadi sasa yanajadili udini na ukabila , na kushauri
kwamba ni vema viongozi wa kila majiji kujitahidi kutumia nafasi hiyo
ili kuondoa matabaka.
“
Watanzania kuna mambo ambayo tulijiwekea tangu enzi za Baba wa Taifa
Mwalimu Julius Nyerere ambapo ndio msingi mkuu tulionao, hakuna ubaguzi
wa dini wala rangi, jambo kama hili ni maeneo machache sana katika Nchi
yetu kuyakuta, hivyo Tanzania tunajivunia kuwa na utamaduni huu” alisema
Meya Mwita.
Alieleza
kwamba “ Jumuiya za kimataifa zimekuwa zikiwatazama waislam wote kama
watu ambao si salama nakushauri kwamba haki za kibinadamu zizingatiwe
kwao kwakuwa wote tunaumbwa na Mungu mmoja” alisema Meya Mwita.
Aliongeza
kwamba “ wapo watu ambao wanaitumia dini ya kiisilamu vibaya,
nakuchafua watu wengine , lakini tunatakiwa kutambua kwamba wote hapa
tumeumbwa na Mungu mmoja, sasa dini zetu zisitufanye tukashindwa
kushirikiana na kuzungumza lugha moja” alisisitiza.
Hata
hivyo katika hatua nyingine Meya alisisitiza majiji makubwa ya nchi za
kiafrika yajielekeze katika kutatua changamoto za watu wake.
Aidha
Meya ametumia nafasi hiyo kuwakaribisha Wairan kuja kuwekeza katika Tanzania sambamba katika kuendeleza fursa za kibiashara.
Hata
hivyo mkutano huo umemalizika jana na kwamba Meya kesho ataelekea
jijini Teheran kwa mwaliko wa Meya wa jiji hilo ambapo pamoja na mambo
mengine huko atatembelea ofisi za umma na kukutana na wadau mbali mbali
kwa ajili ya kujadili namna ya kuendesha majiji sambamba na kutatua
changamoto.
SHARE
No comments:
Post a Comment