Hayawi hayawi hatimaye yamekuwa baada ya Melania Trump na mtoto wake kuhamia Ikulu ya Marekani ya White House ikiwa ni miezi matano tangu mumewe Donald Trump kuingia ofisini.
Hatua hiyo imekuwa ya kushangaza kwa wengi kwa kuwa ndiyo familia ya kwanza miaka ya hivi karibuni kukosa kuhamia Ikulu ya White House mara moja.
- Daily Mail kumlipa Melania Trump kwa kumchafulia jina
- Melania Trump alifanya kazi bila kibali Marekani
- Melania Trump ashtaki kuhusu ukahaba
Hata hivyo inaonekana kuwa Melania amefurahishwa na hatua yake kuhamia White House baada ya kuandika kwenye Twitter alipowasili.
Barron amekuwa akisomea shule ya kibinafsi iliyopo jiji la New York. Trump si rais wa kwanza wa Marekani hivi karibuni kuhamia White House akiwa na watoto wa umri wa kwenda shule.
Rais Barack Obama alipoingia madarakani, mabinti wake Malia na Sasha walikuwa na umri wa miaka 10 na 7. Rais Bill Clinton alipohamia ikulu Washington, Chelsea Clinton alikuwa na miaka 12.
Watoto hao wote walihamia White House masomo ya kiendelea na walihudhuria masomo shule ya Sidwell Friends, shule ya kibinafsi iliyo kaskazini magharibi mwa Washington.
CHANZO: DW
SHARE
No comments:
Post a Comment