TRA

TRA

Wednesday, June 14, 2017

MOTO MKUBWA WASHIKA JENGO LA GOROFA 24 JIJINI LONDON, NI GRENFELL TOWER

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !



NA K-VIS BLOG/Mashirika ya Habari
WATU kadhaa wameuawa na zaidi wengi 50 kujeruhiwa kutokana na moto mkubwa ambao umezuka kwenye jengo la ghrorofa 24 Grenfell Tower la makazi ya watu jijini London, Uingereza leo Jumatano Juni 14, 2017.
Meya wa jiji hilo Mstahiki Sadiq Khan amesema idadi kubwa ya watu wamejeruhiwa na watu wengine ambao idadi yao haijajulikana wameuawa.
Kikosi cha zimamoto na uokoaji jijini London, kimetuma kwa uchache wahandisi wa moto 40, magari ya kubeba wagonjwa, (Ambulance), zipatazo 20 na zaidi ya askari wa zimamoto na uokoaji wapatao 200.
Mwakilishi wa kikosi cha zimaoto na uokoaji jijini London amesema kuna idadi kubwa ya waliokumbwa na kadhia hiyo ya moto lakini amekataa kusema ni watu wangapi wameuawa.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger