Watu nchini
Indonesia wameungana kumsaidia mzee mmoja muuza ndizi ambaye anasema
kuwa aliiporwa zaidi ya rupiah milioni 1 au dola 80.
Tommy Reza alichapisha video ya Bwana Suratman akiwa mwenye mawazo ambayo imevutia huruma na watu kutoa mchango.
Kisa hicho kilitokea mkoa wa Jambi katika kisiwa cha Sumtara. Tommy Reza aliambia BBC kuwa alimpata Bwana Suratman akiwa mwenye majonzi.
"Nilikuwa eneo hilo wakati nilimuona mwanamume akipiga kelele akiomba msaada," alisema Reza.
Tangua video hiyo iweke kwenye mitandao ya zaidi ya rupiah milioni 37, zaidi ya dola 2900 zimechangwa.
Gavana wa eneo hilo baadaye alitoa rupiah milioni 5. Kisha bwana Reza akachapisha picha akimkabidhi Suratman pesa hizo.
CHANZO: BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment