TRA

TRA

Thursday, June 22, 2017

Mzimu wa FBI wazidi kumtesa Rais Trump

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !



Rais wa Marekani Donald Trump amesema hakumrekodi aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa shirika la FBI James Comey licha ya kudai hivyo hapo awali.

Alituma ujumbe katika mtandao wake wa Twitter kwamba hakutengeza na wala hana rekodi hizo siku moja baada ya kutakiwa kuwasilisha kanda hizo kwa jopo la Congress.

Bwana Trump alianzisha uvumi wa rekodi hizo katika ujumbe wa Twitter aliochapisha siku moja baada ya kumfuta kazi bwana Comey mnamo mwezi Mei.

Alisema: James Comey uwe na matumaini kwamba sina sina rekodi zozote za sauti yako kuhusu mazungumzo yetu.

Chapisho hilo lilizua madai chungu nzima kwamba bwana Comey alifutwa kazi ili kuzuia uchunguzi kuhusu Urusi kuingilia Uchaguzi wa Marekani mwaka uliopita mbali na ushirikiano wake na kampeni ya rais Donald Trump mjini Moscow.


 Donald Trump na aliyekuwa mkurugenzi wa shirika la ujasusi nchini Marekani FBI James Comey

Licha ya lengo lake kutobainika, ujumbe huo wa Twitter ulisababisha kuajiriwa kwa mtaalam ambaye amechukua uongozi wa uchunguzi wa madai hayo.

Swala hilo linatokana na uchaguzi wa urais wa mwaka jana na ushahidi unaotolewa kwamba wadukuzi wa Urusi walilenga mifumo ya uchaguzi ya Marekani kwa lengo la kumsaidia Donald Trump kushinda kitu ambacho Moscow inakana.

CHANZO: BBC

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger