Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za
uwekezaji Bw. John Mnali akizungumza na waandishi wa habari wakati wa
mafunzo hayo leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wajasirimali wakifuatilia mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC).
Mmoja wa wajasiriamali hao Bibi Neli William akishukuru TIC kwa kuandaa mafunzo hayo.
(Picha na Frank Shija)
………………………………………………………………..
Frank Mvungi-Maelezo
Kituo cha Uwekezaji Tanzania
(TIC) kimewataka Wajasiriamali nchini kujiamini na kutumia fursa
zilizopo ili kukuza biashara zao na kuchochea ukuaji wa uchumi.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za
Uwekezaji wa TIC, Bw. John Mnali AMETOA WITO HUO wakAti wa mafunzo ya
siku moja kwa wajasiriamali yaliyolenga kuwajengea uwezo wa kuzalisha
bidhaa zinazokidhi mahitaji ya soko kwa kuzingatia ubora.
Akifafanua Mnali amesema mafunzo
hayo ni fursa kwa wajasiriamali wakati na wadogo kukutana na
wajasiriamali wakubwa waliowekeza hapa nchini hali itakayochochea
kuongeza ubora wa bidhaa na huduma wanazotoa.
“Jukumu la Kituo cha Uwekezaji
hapa nchini ni kuhakikisha kuwa wajasiriamali wadogo na wakati
wanazalisha bidhaa zitakazotumiwa na makampuni makubwa ya wawekezaji”,
alisisitiza Mnali
Katika kuhakikisha kuwa
wajasiriamali wanakuza mitaji yao Kituo cha Uwekezaji kimeshirikisha
taasisi za fedha katika mafunzo hayo ili kuwapa fursa wajasiriamali
wadogo na wakati kupata mikopo itakayo wawezesha kukuza uzalishaji wao.
Kwa upande wake mmoja wa
wajasiriamali hao, Bi. Neli William amesema kuwa wajasiriamali
Watanzania wamekuwa waoga kudhubutu kuzalisha bidhaa kwa wingi na
kuzitangaza ili kukuza soko la bidhaa hizo.
“Nakishukuru Kituo cha Uwekezaji
Tanzania kwa mafunzo haya kwa kuwa yametujengea uwezo ambao utasaidia
kukuza uzalishaji wetu na kuongeza tija”, alieleza Bi. Neli.
Aliongeza kuwa kila siku anao
uwezo wa kuzalisha trei 70 za mayai hivyo baada ya mafunzo dhamira yake
ni kuongeza kiwango cha uzalishaji.
Kituo cha uwekezaji Tanzania
(TIC) kimekuwa kikitoa mafunzo kwa wajasiriamali hapa nchini ili
kuwajengea uwezo wa kuzalisha bidhaa zenye ubora kulingana na mahitaji
ya soko.
SHARE
No comments:
Post a Comment