Napenda
kuungana na mamilioni ya Watanzania kumpongeza Rais wa Jamhuri Muungano
Tanzania Dk. John Pombe Magufuli kutokana na uzalendo, uthubutu na
ujasiri aliouonyesha katika katika kulinda rasilimali zetu zimnufaishe
Mtanzania.
Watanzania
tulio wengi tunashindwa mambo kuyafanya kutokana na kukosa ushupavu wa
uthubutu katika kuamua kuyafanya mambo. Hakuna jambo lililowahi
kufanikiwa bila ya kuwepo kitu uthubutu. Uthubutu ndio mwanzo wa
mafanikio ya jambo lolote lile.
Mwalimu
Nyerere alijizatiti akiwa na malengo ya kupigania Uhuru wa Tanganyika
wakati akijua fika kuna mkoloni Mwingereza aliyekuwa akitawala lakini
alitanguliza mbele uthubutu wa kuweza jambo na hatimaye mnamo Disemba 9,
1961 malengo yake yalitimia.
Miaka
ya 1980's kuliibuka genge kubwa la wahujumu uchumi nchini ambao
walificha bidhaa ili waje wazilangue. Kuliibuka mafisadi wa kiuchumi
ambao walikuwa na nguvu iliyopitiliza ya kuogopwa lakini akaibuka Ndugu
Edward Moringe Sokoine kupambana nao vikali kwa kutanguliza uthubutu
kwanza na hatimaye wahujumu uchumi wenyewe wakaanza kutoa mafichoni Mali
na bidhaa walizozificha kutokana na kuibuka kiongozi shupavu na jasiri
aliyekuwa na uthubutu wa kukabiliana nao. Hatimaye Sokoine alifanikiwa
kushinda vita dhidi yake na wahujumu uchumi.
Hayo
yote ni matokeo ya uthubutu. Leo hii ameibuka kiongozi mwingine Rais
Dk. John Pombe Magufuli ambaye ni mfano bora wa kuigwa kutokana na
kutanguliza mbele uzalendo na uthubutu wa kupambana na wahujumu
rasilimali zetu na yupo tayari kuzilinda.
Uzalendo
wa Rais Magufuli ulianza kwa kuzuia makontena 277 yenye mchanga wa
madini yasisafirishwe kwenda nje na kuunda tume mbili ambazo zimetufunua
macho juu ya matrilioni ya pesa tuliyokuwa tunaibiwa.
Watanzania
hatukupaswa kabisa kuwa maskini, kukosa madawa hospitalini, kukosa
miundombinu bora, kuwa na Kilimo duni huku tukikosa pembejeo, kula
mmoja. Watanzania hatukustahili maisha ama maumivu haya.
Waliotufikisha
hapa Rais Magufuli amewafuta kazi, ameagiza walio nje ya madaraka
waanze kuhojiwa Mara moja. Na kauli ya Rais inakwenda mbali zaidi ya
hapo kwamba hawataishia kuhojiwa tu bali watapandishwa mahakamani.
Kwa
muda mrefu tumekuwa tukilalamika tukiibiwa madini, tumekuwa
tukilalamika rasilimali zetu hazitunufaishi Watanzania. Tulikosa kabisa
jasiri Mzalendo wa kuanzisha vita hii ya ukombozi wa kiuchumi.
Naupongeza
uzalendo na uthubutu aliouonyesha Rais Magufuli. Sasa ni wajibu wetu
kama Taifa kuungana kwa pamoja ili kuziokoa rasilimali zetu zitunufaishe
sote na vizazi vyetu.
Emmanuel John Shilatu
12/06/2017
0767488622
SHARE
No comments:
Post a Comment