Wanaharakati katika jimbo la
Arkansas nchini Marekani, wanapinga ujenzi wa jiwe moja kubwa lililo na
maandishi ya amri 10 za Mungu, kwenye uwanja wa makao makuu ya bunge la
jimbo hilo.
J
Muungano wa Haki na Uhuru wa raia Marekani (ACLU), umewasilisha kesi mahakamani kutaka kuondolewa mara moja kwa mnara huo, ukisema unaleta mgawanyiko na unakiuka ahadi ya uhuru wa kidini kwa wote, katika katiba ya Marekani.
Seneta wa Chama Tawala cha Republican, Jayson Rapert, ambaye alikuwa katika mstari wa mbele wa kutaka kuwekwa kwa jiwe hilo , alisema kuwa hatua hiyo inaenda sambamba na msimamo wa mahakama kuu ya Marekani, na hivyo ni jambo zuri kwa jimbo la Arkansas.
SHARE
No comments:
Post a Comment