Watafiti wa usalama
wamegundua chanjo ya shambulio la uhalifu wa mitandaoni lililoathiri
mashirika tofauti duniani siku ya Jumanne.
Wataalam bado hawajui shambulio hilo linatoka wapi na lengo lake ni nini.Huku ikidaiwa kwamba kikombozi inachotaka ni cha kiasi kidogo cha dola 300, wengi wanadai shambulio hilo linaweza kusababisha madhara mabaya zaidi ama hata kutoa tamko la kisiasa.
- Microsoft: Shambulizi la Kompyuta liwe funzo
- Marekani yachunguza shambulio kubwa la mtandao
- Shambulizi la uhalifu wa mtandao laathiri mataifa 99 duniani
Pia waliopatikana katika shambulio hilo ni hospitali moja ya Marekani katika mji wa Pittsburgh.
Lakini kwa wale walio na wasiwasi kuhusu shambulio hilo,kunaonekana kuna dawa inayoweza kudhibiti athari za kiini hicho.
Kwa kutengeneza faili kwa jina Perfc na kuiweka katika "C:\Windows" folder, shambulio linaweza kusitishwa mara moja.
Maelezo ya kufanya hivyo yamechapishwa katika kompyuta ya usalama na kusaidiwa na wataalam wengine.
Hata hivyo huku mbinu hiyo ikiwa ina uwezo wa kudhibiti kirusi hicho, ina uwezo wa kuzilinda kompyuta za kibinafsi ambazo faili zina Perfc.
Watafiti kufikia sasa wameshindwa kupata suluhu ya kudumu itakayozuia shambulio hilo kabisa.
Ijapokuwa inaweza kuifanya mashine kuwa na kinga kama alivyoelezea mwanasayansi wa kompyuta Profesa Alan Woodward, bado inaweza kusambaza kiini hicho katika kompyuta nyengine zilizounganishwa.
Kwa watumizi wengi, kuweka Windows mpya ni suluhu ya kuzuia shambulio hilo iwapo ingetaka kuathiri komyuta yako.
Kusambaa kwa kirusi hicho kipya kunaweza kuwa kwa mwendo wa pole ikilinganishwa na kile cha mwezi ulioipita cha WannaCry wataalam wametabiri huku wachangunuzi wa alama za siri wakisema kuwa kirusi hicho hakikuwa na lengo la kusambaa zaidi ya lengo lake.
CHANZO: BBC
Kutokana na hilo, wataalam kadhaa wanatabiri kwamba shambulio hilo halitasambaa sana kama lilivyofanya siku ya Jumanne hadi pale kiini hicho kitakapoimarishwa.
SHARE
No comments:
Post a Comment