BANKI ya NMB imefanikisha kufanyika kwa Tamasha maalum la watoto ‘Mtoto Day Out’ kwa kuwa mdhamini mkuu wa Tamasha hilo. Tamasha hilo ambalo limekutanisha watoto wa maeneo mbalimbali ya jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na kufurahi pia wamepata elimu kuhusu umuhimu wa kutunza fedha. Akizungumza na MO Blog kuhusu tamasha hilo, Mratibu wa Elimu ya Fedha wa benki ya NMB, Ryoba Mkono alisema NMB imedhamini tamasha hilo ili watoto wafurahi lakini pia wapate elimu kuhusu fedha na umuhimu wa kuzitunza.
Mkono alisema pamoja na mambo hayo pia NMB ilitoa ofa ya watoto kufunguliwa akaunti ya Mtoto na Chipukizi akaunti bure kwa watoto waliohuddhuria tamasha hilo lakini pia kuwapa zawadi za aina mbalimbali ambazo walikuwa wamewaandalia kwa siku hiyo.
“Sisi kama wadhamini wa Mtoto Day Out NMB tumewaletea elimu ya fedha na umuhimu wa kuweka akiba lakini pia kuwafungulia watoto akaunti bure lakini pia imekuwa njia bora ya kukutana na wazazi maana tumekuwa tukikutana na watoto mashuleni lakini wazazi hatukutani nao,
“Lakini pia sababu NMN inathamini elimu tumeamua kununua madaftari yenye logo ya NMB, karamu, rula, mabegi, penseli kwa ajili ya watoto na zawadi zetu zinaandana na elimu,” alisema Mkono.
Kwa upande wa mmoja wa waandaji wa tamasha hilo, Glory Shayo alisema dhumuni la kuandaa tamasha hilo ni kukutanisha watoto wafurahi kwani wao huwa hawapati nafasi ya kutoka tofauti na wazazi hivyo siku hiyo ilikuwa muhimu kwa ajili yao na wao kufurahi kwa pamoja na kupata elimu ya fedha kutoka NMB.
“Tumeanda tamasha kwa ajili ya watoto, wazazi tuna out nyingi muda mwingine tunawapeleka kwenye sehemu za wazazi lakini wanakpata wapi muda wa kukutana, muda wa kujifunza na kushiriki michezo na wenzao? ni changamoto ni vema wakipata nafasi ya kukutana na kucheza kwa pamoja na kupitia NMB tukaandaa hii Mtoto Day Out,” alisema Glory.
SHARE
No comments:
Post a Comment