Moja
kati ya maswali ambayo yamekuwa yakikosa majibu kwenye vichwa vya watu
wengi ni pamoja na hili la ngoma za wasanii ambao wamekuwa
wakiwashirikisha wasanii kutoka WCB, video za ngoma hizo kuwa zinakaa
kwenye Youtube Chanel za wasanii hao wa WCB na si wamiliki wa ngoma
hizo kama ilivyo kawaida.
Tukianza na Inde ya Prince Dully Sykes aliyomshirikisha Harmonize, tukija kwa Stereo na ngoma yake ya Mpe Habari aliyomshirikisha Rich Mavoko na hata hii ya Unaionaje ya Young Killer ambayo imedropishwa wiki iliyopita amemshirikisha Harmonize.
Young Killer na kupiga naye story kuwa imekuaje kiupande wake video ya ngoma yake kukaa kwenye Youtube Chanel ya Harmonize ikiwa inafahamika fika kuwa mtonyo wa Youtube ndio kitu ambacho kinatolewa macho na wasanii weng kwa sasa.
Young Killer ameiambia Perfect255 kuwa
kwa upande wake hajawahi kunufaika kwa chochote kutoka kwenye Youtube
Chanel yake na ndio sababu ya video yake hiyo kukaa kwenye chanel ya Harmonizeangalau iweze kupata nguvu na kuingiza chochote kitu katika suala zima la mtonyo.
“Kiukweli
Youtube imekuwa ni chanzo kikubwa cha kuwaingizia watu hela kwa kiasi
kikubwa sana, lakini mimi binafsi sijawahi kunufaika chochote kupitia
Youtube.” Alisema Young Killer.
Pia Young Killer aliongeza kuwa video ya “Unaionaje”
ni video kubwa iliyogharimu pesa nyingi zaidi kwahiyo inahitaji angalau
ipate chochote kile ili watu waweze kunufaika kwa kile ambacho
wamekifanya, ukizingatia chanel ya Harmonize ni chanel iliyosajiliwa na inaingiza pesa nyingi.
SHARE
No comments:
Post a Comment