Waziri Mkuu wa
Iraq, Haider al-Abadi, ametembelea mji wa Mosul kuwapongeza wanajeshi
katika kile alichokiita ukombozi wa mji huo kutoka kundi la wapiganaji
wa Kiislamu.
Waziri mkuu wa Iraq awasili mji uliokombolewa wa Mosul
Muungano wa majeshi ya Marekani yaukomboa mji wa Mosul
Raia 50 wameuwawa Mosul, Iraq
Mosul ndipo kundi la wapiganaji wa kiislamu IS lilipotangaza kuunda uongozi wake miaka mitatu iliyopita.
Sehemu kubwa ya mji huo imekuwa vifusi baada ya mapigano ya miezi tisa ya kuwaondoa wapiganaji hao. Abadi amekuwa akitembea katika barabara za mji wa Mosul na kuwapongeza wanajeshi.
Wakati huo huo, kumekuwa na sherehe pindi alipozuru eneo hilo.
Mwanzoni kulikuwa na taarifa za kuwepo mapigano, na moshi mzito ukionekana juu ya eneo ambao limekuwa ndio kitovu cha wapiganaji wa IS.
Kundi hilo bado linahodhi sehemu ya magharibi na Kusini mwa Mosul na inaaminika litaendelea kufanya mashambulizi katika sehemu kubwa ya Iraq.
Wapiganaji waliuteka mji wa Mosul mwezi June mwaka 2014. Vikosi vya Iraq, vikisaidiwa na mashambulio ya anga kutoka Marekani, vimekuwa vikipambana kuirudisha Mosul tangu tarehem 17 mwezi Oktoba mwaka jana.
Maelfu ya raia wamekimbia huku wengine wakikosa pa kukimbilia wakati mapigano yakiendelea.
SHARE
No comments:
Post a Comment