Viongozi wa kundi la mataifa ya G20
wamekubaliana katika kulaani ghasia zilizofanywa na
waandamanaji mjini hamburg lakini wameshindwa kuja pamoja katika mawazo
yao kuhusiana na mabadiliko ya tabia nchi na biashara huru.
Anaandika mwandishi wa DW ,Bernd Roegart kutoka Hamburg kwamba
kansela Angela Merkel ambaye alikuwa mwenyeji wa mkutano huo
wa kilele alijitokeza katika tukio maalum mwishoni mwa mkutano
huo wa G20, wakati alipokutana na wawakilishi wa jeshi la polisi.
Aliwashukuru kwa kuweka maisha yao katika hatari kuhakikisha
usalama kwa viongozi wa nchi na serikali pamoja na wajumbe
wao wakati wakikutana katika mji huo wa kaskazini mwa Ujerumani.Kansela wa Ujerumani hakutafuna maneno katika shutuma zake kali dhidi ya mapambano ya ghasia ambayo wanaharakati wanaopinga utandawazi walipambana katika siku mbili hapo kabla. "Watu ambao wanafanya hivyo hawana nia ya kukosoa masuala ya siasa. Wale wanaofanya hivyo wanafanyakazi nje ya jamii ya kidemokrasi." Merkel pia aliahidi msaada wa haraka kwa wahanga wa vitendo vya ghasia.
Marais katika eneo la Schanzen mjini Hamburg na vitongoji vya Altona hawakuwa na hamasa juu ya kazi iliyofanywa na polisi. Vitongoji hivyo vilikuwa ni uwanja wa mapambano na uporaji na uchomaji moto dhidi ya biashara mbali mbali , vitendo vilivyofanywa na waandamaji waporaji , magari kadhaa yaliharibiwa pia.
Mkaazi mmoja ambaye alifadhaishwa aliweka bango kubwa kutoka katika varanda yake lililosomeka: "hiyo ilikuwa ni wazo la kijinga Olaf." Olaf ni Olaf Scholz, meya wa sasa wa mji wa Hamburg. Anahisika na kuuleta mkutano wa G20 mjini Hamburg na aliwaahidi wakaazi kwamba usalama wao utahakikishwa wakati alipozungumzia wasi wasi wao kabla ya mkutano huo.
Usalama wahakikishwa
Hakuna muandamanaji aliyeweza kufika katika eneo lililotengwa kwa ajili ya mkutano huo , ambako viongozi wa mataifa 19 yenye utajiri mkubwa wa viwanda pamoja na yale yanayoinukia kiuchumi pamoja na wawakilishi kutoka Umoja wa Ulaya walikutana siku ya Ijumaa na Jumamosi.
Jaribio lolote kufanya hivyo lilizuiwa na polisi wapatao 20,000 na majeshi ya usalama kutoka Ujerumani na mataifa jirani ya Umoja wa Ulaya.Ndani ya jengo la maonesho ya biashara ambako mikutano ilifanyika, taarifa ya mwisho ya pamoja iliwasilishwa ambayo ilibakia kuwa haieleweki katika maeneo mbali mbali.
Mataifa yote 20 yalikubaliana kwa pamoja katika imani yao kwamba utaratibu wa kudhibiti masoko ya fedha uendelee, pamoja na haja ya kupambana na hali ya kufadhili ugaidi na ukwepaji kodi. Masuala haya ni msingi wa wasi wasi wa "serikali za dunia" ambao uliasisiwa kama jibu kwa mzozo wa kifedha wa mwaka 2008.
Umoja , ambao ni utamaduni wa kundi la G20 , ulifikia mwisho , hata hivyo , katika mada ya kupambana na ongezeko la ujoto duniani. Idadi ya waliokubali ilikuwa 19 dhidi ya mmoja , kwa kuwa Marekani hivi karibuni ilijitoa kutoka makubaliano ya Umoja wa mataifa ya mjini Paris kuhusiana na mabadiliko ya tabia nchi.
Mjini Hamburg , rais wa Marekani Donald Trump pia alikataa kutambua upunguzaji wa utoaji gesi hizo zinazochafua mazingira uliomo katika makubaliano ya Paris.
Marekani yashikilia msimamo wake
"Kila palipo na muafaka, ni lazima pia kuna mpinzani," kansela Angela Merkel alisema, na kuongeza kwamba anasikitishwa na ukweli kwamba Marekani imeachana na muafaka wa mazingira. "Nafarijika kwamba kila kiongozi mwingine wa taifa na serikali anakiri kwamba makubaliano ya Paris hayawezi kubadilishwa."
Merkel amesisitiza kwamba makubaliano yanapaswa kutekelezwa haraka iwezekanavyo. Trump alitoa taarifa ambayo iliongezwa katika taarifa ya mwisho ya pamoja na kusema kwamba Marekani inataka kusaidia mataifa mengine kupata njia salama za kutumia nishati za makaa ya mawe , gesi na mafuta. Makubaliano ya Paris yanataka kusitishwa kabisa kwa matumizi hayo.
Katika mada ya biashara, wajumbe wa majadiliano wa G20 walitumia siku kadhaa wakipambana na upinzani wa Marekani kabla ya hatimaye kufikia makubaliano. Hatimaye , mkutano huo wa kilele ulikubaliana kuhusu biashara ya haki kwa wote na kuonesha nia ya kuimarisha taasisi ambazo zinaweza kutumika wakati ambapo biashara imekwazika.
Kama ilivyokuwa hapo kabla , shirika la biashara duniani WTO litakuwa kama muamuzi. Uwezo wa kuingia katika masoko ulitajwa pia. Suala hilo liliongezwa kwa kuiangalia zaidi China , ambayo inataka kulinda sana makampuni yake dhidi ya ushindani nyumbani na wawekezaji wa kigeni. Donald Trump alijitokeza dhidi ya makubaliano ya biashara yanayohusu makundi ya mataifa , kwasababu alisema "hayatendi haki" kwa Marekani.
Anataka makubaliano ya nchi moja moja, kama vile na Uingereza, ambayo inakaribia kujitoa kutoka Umoja wa ulaya katika muda wa miaka miwili ijayo.
Kuhami masoko
Hata hivyo kinyume na taarifa nyingi zilizotolewa hadi sasa, Trump alisema haamini kuhusu kuhami masoko. Kwa hiyo hii inaonekana kama ushindi mdogo kwa kundi la G20. "tunaweza kufanikiwa zaidi wakati tukichukua hatua kwa pamoja kuliko ukichukua hatua peke yako," amesema kansela Merkel.
Kansela Merkel pia amefanikiwa katika kusukuma wazo ambalo analipenda sana. G20 ikubaliane kufanya uwekezaji mpya kwa Afrika. matumaini ni kwamba uwekezaji wa moja kwa maja wa mashirika utatia nguvu uchumi wa mataifa ya Afrika.
G20 inasema pia kwamba inataka kulisaidia bara la Afrika kutumia na kuwezesha uwekezaji kwa kuyapatia mataifa hayo fedha za kuanzia. Ni matumaini kwamba muktadha mpya wa kiuchumi utawafanya watu wa Afrika waache kuhamia katika bara la Ulaya. Na hii ni kupitia kile kinachofahamika kama "Mkataba na Afrika" ambao umekuwa sehemu ya mkakati wa Umoja wa Ulaya wa kupambana na uhamiaji.
Hata hivyo , kuna sehemu kubwa ya kuweza kuboreshwa. Kwa hivi sasa , Uwekezaji wa Ujerumani katika bara la Afrika unafikia tu kiasi cha asilimia moja ya jumla ya uwekezaji wa kibiashara za kigeni za Ujerumani. Taasisi za serikali za China zinaongoza dunia katika uwekezaji wa moja kwa moja katika Afrika na haipotezi muda mwingi ikitia shaka juu ya masuala ya utawala bora katika bara hilo.
SHARE
No comments:
Post a Comment