TRA

TRA

Tuesday, July 4, 2017

Kutakatisha fedha maana yake ni nini?

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !

 


Tumesikia watu wanafungwa kwa kutakatisha fedha, wengine kuhujumu uchumi, sasa leo tumempata mtaalamu kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Meneja Msaidizi Idara ya Uendeshaji kesi na uchunguzi, Ganga Mlipano kwenye huu ufafanuzi.

CHANZO: Millardayo.com

"Nchi yoyote inatakiwa kuwa na uchumi imara vitendo vyovyote vinavyofanya uchumi usiwe imara ni vitendo vinavyofanya uchumi uhujumiwe ndiyo maana Serikali yetu ilitunga sheria ya uhujumu uchumi mwaka 1984.

"Vitendo vyote vinavyofanywa ambavyo vimeelezewa kwenye hiyo sheria vinavyopelekea kuhujumu uchumi vinaitwa vitendo vya kuhujumu uchumi na mtu yeyote akifanya hivyo vitendo anapelekwa Mahakamani na kushtakiwa.

"Ili uchumi uendelee lazima kuwe na mtiririko wa fedha, mtu anapochukua fedha akaweka nyumbani au akachukua bidhaa nyingi za kiasi kikubwa akazihifadhi nyumbani na wananchi wakakosa maana yake kutatokea mfumuko wa bei. Vitendo kama hivyo ndiyo hupelekea uchumi uyumbe.

"Vitendo vinavyopelekea masuala haya ndio vinaitwa vitendo vya kuhujumu uchumi. Na kuhusu kutakatisha fedha…fedha kwa kawaida inatakiwa kutumika kama ilivyopangwa. Mtu anaweza kupata fedha kwa njia si ya halali na akaitakatisha," anasema.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger