Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli ameiagiza
Wizara ya Nishati na Madini kusitisha utoaji wa leseni mpya za uchimbaji
halikadhalika leseni ambazo zimeisha muda wake.
Rais
Magufuli ametoa maagizo hayo alipokuwa akizungumza na wananchi wa Geita
ambao walizuia msafara wake katika maeneo mbalimbali wakati akiwa njiani
kuelekea Chato.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, jana tarehe 4 Julai, 2017 amehitimisha ziara yake ya kikazi ya Siku Mbili
Mkoani Mwanza kwa kuzindua mradi wa Uboreshaji wa huduma ya Maji Safi na
Usafi wa Mazingira katika kijiji cha Nyamazugo Wilayani Sengerema.
Mradi huo
wa maji umetekelezwa chini ya mpango wa maji wa Kamisheni ya Bonde la
Ziwa Victoria ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa ufadhili wa Benki ya
Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa gharama ya shilingi bilioni 22.4.
Mradi
wa Maji Safi mjini Sengerema ulioanza tangu mwaka 2011 unatarajiwa
kuwahudumia wakazi 138,000 ifikapo mwaka 2030.
Akizungumza
katika hafla ya uzinduzi wa Mradi huo, Mhe. Rais Dk. Magufuli amesema
kukamilika kwa mradi huo kutamaliza tatizo la maji la muda mrefu kwa
wakazi wa Sengerema na maeneo ya jirani.
Rais
Dkt. Magufuli amewataka wananchi wanaozunguka mradi huo kuutunza na
kuhakikisha hawaharibu vyanzo vya maji katika eneo hilo la ziwa Victoria
ikiwa ni pamoja na kuacha uvuvi haramu ambao umekuwa na madhara makubwa
kwa wananchi.
Aidha,
ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Mwanza na Vyombo vya Dola kuchukua hatua
kali dhidi ya watu wanaochafua vyanzo vya maji katika eneo la Ziwa
Victoria.
Katika
hafla hiyo ya Uzinduzi wa mradi wa maji Kada wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo – CHADEMA HamisiHussein Maarufu TABASAM, ameamua kuachana na
chama chake na kujiunga na CCCM.
Mhe. Rais
Dk. Magufuli ameendelea kusisitiza msimamo wa Serikali kuwa hakuna
mwanafunzi atakayepata ujauzito ataruhusiwa kuendelea na masomo na
ameyataka Mashrika yasiyo ya Kiserikali ambayo yamekuwa yakipinga uamuzi
huo kufungua Shule zao wenyewe ambazo zitawasomesha wanafunzi wanaopata
ujauzito.
“Haiwezekani
Serikali itoe pesa kuwasomesha wanafunzi halafu wapate mimba waendelee
na masomo hilo haiwezekani, hizo NGOs zinazotetea hali hiyo zikitaka
zijenge shule kwa ajili ya kuwasomesha wanafunzi watakaopata
ujauzito," amesema Rais Magufuli.
Rais
Magufuli amezungumzia uamuzi wa Serikali kupeleka Miswada Mitatu ya
dharura Bungeni kuwa unatokana na umuhimu wa hilo katika kutetea maslahi
mapana ya nchi na kuhakikisha rasilimali za nchi zinawanufaisha
wananchi.
Rais
Magufuli amewaonya wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM wenye nia ya
kugombea nafasi mbalimbali katika Uchaguzi wa Chama hicho kutojihusisha
na rushwa kwa vile rushwa ni adui wa haki, hivyo, atakayebainika kutumia
rushwa atapoteza sifa ya kuwa Mgombea.
Akizungunzia
ujenzi wa barabara ya kutoka Kamanga hadi Sengerama kwa kiwango cha
lami, Mhe. Rais Dkt. Magufuli amesema kwa sasa Serikali imeshampata
mkandarasi kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu na usanifu ili
barabara hiyo ianze kujengwa katika kutimiza ahadi aliyoitoa wakati wa
kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
Rais
Magufuli pia amewataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya nchni kufafanua kwa
wananchi na kusimamia uamuzi wa Serikali wa kufuta tozo zaidi ya 80
katika mazazo ya Kilimo, tozo 7 za Mifugo na tozo 5 za Uvuvi ambao lengo
lake ni kuwaondolea kero wananchi.
Aidha,
amesema Serikali inafanya uchambuzi ili kubaini wale wote waliotoa
pembejeo hewa na atakayebainika atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Wakati
huo huo, Mheshimiwa Rais Magufuli ameiagiza Wizara ya Nishati na Madini
kusitisha utoaji wa leseni mpya za uchimbaji na halikadhalika leseni
ambazo zimeisha muda wake. Ametoa maagizo hayo alipokuwa akizungumza na
wananchi wa Geita ambao walizuia msafara wake katika maeneo mbalimbali
wakati akiwa njiani kuelekea Chato.
Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Sengerema,Mwanza
04 Julai 2017.
SHARE
No comments:
Post a Comment