
Ni taarifa njema kwa watanzania
wote hususan wadau wa soka kwamba, nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta
upasuaji wake wa goti umefanyika na kumalizika salama.
Samatta aliumia goti November 4,
2017 wakati akiitumikia klabu ya ya KRC Genk ya Ubelgiji na kushindwa
kuendelea na mechi dhidi ya Lokeren mchezo ambao ulimalizika kwa suluhu.
Kupitia ukurasa wake rasmi wa wa instagram (samagoal77) ameandika ujumbe unaothibisha kwamba upasuaji umefanyika na kumalizika salama.
“Napenda kuwajulisha kuwa,
upasuaji wangu umeenda vizuri. Napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu, timu
ya madaktari pamoja na mashabiki wangu.”
“Nimepokea meseji nyingi sana
kutoka sehemu tofauti duniani na napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru
sana kwa meseji na Dua zenu.”
Baada ya kufanyiwa vipimo,
madaktari walimwambia Samatta atakaa nje ya uwanja kwa takribani wiki
sita kabla ya kuanza kucheza tena.
SHARE








No comments:
Post a Comment