Rais
John Magufuli ameukumbuka mchango wa marais wastaafu, Benjamin Mkapa na
Jakaya Kikwete na kuwashukuru huku akieleza kuwa wao ndiyo
waliotengeneza maisha yake ya kisiasa hadi kuwa kiongozi.
Magufuli
ameyasema hayo leo Jumatatu, Julai 10 wilayani Chato wakati wa uzinduzi
wa nyumba 50 zilizojengwa na Taasisi ya Mkapa Foundation.
“Nakumbuka
siku hiyo tulikuja hapa Chato na wewe (Mkapa) Msafara ulisimamishwa na
ukawaambia wananchi wa Chato nichagulieni huyu, nakumbuka ulikuwa umevaa
viatu vyekundu,” alisema na kuongeza:
“Kwa
bahati nzuri, wananchi wa Chato wakanichagua, baadaye ukanichagua kuwa
naibu waziri. Wewe ulinitangaza, sikustahili chochote, maneno yako
yalikuwa na nguvu kwa Watanzania.”
Alisema anamkushukuru pia Rais Mstaafu Jakaya Kkwete na kusema:
“Baada ya kipindi cha Mkapa, Kikwete alipokuja, lakini kwanza wewe
ukanipitisha kugombea ubunge tena kwa mara nyingine, nikachaguliwa bila
kupingwa katika jimbo hili.” Amesema
Alisema hata katika kipindi cha awamu ya nne, Rais Kikwete alimteua katika wizara mbalimbali.
“Kwangu
mimi nyinyi mlitengeneza maisha yangu katika uongozi. Pia nawashukuru
sana viongozi wa awamu ya kwanza, Nyerere na Mwinyi ambao walitengeneza
mazingira mazuri ndani ya Chama cha Mapinduzi,” amesema na kuongeza:
“Kwangu
mimi sina cha kuwalipa jukumu langu ni kuwatetea na ninawaahidi
Watanzania kuwa nitafanya kazi kwa nguvu zangu zote, namuomba Mungu
asinifanye nikawa na kiburi namuomba asinifanye nikasahau nilipotoka.”
SHARE
No comments:
Post a Comment