Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli amesema amepata
mialiko zaidi ya 60 hajaenda kwa sababu anataka kushughulika na matatizo
ya Watanzania.
Rais ameyasema hayo leo alipokuwa akihutubia wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji Sengerema.
“Nimeshapata
mialiko zaidi ya 60 ila sijaendi, Nikienda huku najua watapiga Watanzania wajanja sana. Hizo safari zipo tu, hata nikistaafu nitaenda.
Wacha nishughulikie matatizo ya watanzania kwanza,” alisema Rais
Magufuli.
Rais Magufuli yupo mkoani Mwanza kwa ziara ya siku mbili.
SHARE
No comments:
Post a Comment