Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli amezitaka Asasi za
Kiraia (NGO’s) kufungua shule kwa wanafunzi wanaopata mimba shuleni kama
kweli zinawapenda wanafunzi hao.
Rais Dk. John Magufuli
Rais amesema hayo leo Jumanne, Julai 4 alipokuwa akihutubia wananchi wa wilaya ya Sengerema wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji.
“Si
kwamba nawachukia wenye mimba, hata kwa bahati mbaya akapata mimba, kama
hizo NGO zinawatetea sana, zifungue shule za wenye mimba, kwa sababu
zinawapenda wenye mimba, wafungue shule zao,”alisema Rais Magufuli huku
akiendelea kusisitiza kuwa.
“Haiwezekani
fedha za walipa kodi, Sh 17 bilioni kila mwaka za kusomesha watoto
wetu, kwenda kusomesha wakinamama, wazunguke, waimbe, waseme nini mimi
ndiyo Rais, huo ndio ukweli,” alisema Rais Magufuli.
Hata
hivyo, Rais Magufuli tatizo si wanaopata mimba, kwani wapo waliopata
matatizo, kama kuugua kwa muda mrefu wakashindwa kwenda shule lakini
ulianzishwa mpango maalum wa kuwasomesha katika mfumo usio rasmi.
SHARE
No comments:
Post a Comment