Mahakama
Kuu ya Tanzania imesema inatarajia kuanza kusikiliza maombi ya dhamana
yaliyotolewa na Mfanyabiashara maarufu Tanzania Yusuf Manji, August 4,
2017.
Jaji
Isaya Arufani amesema hayo jana baada ya Mawakili wa Serikali Paul
Kadushi na Simon Wankyo kuyapokea maombi hayo na kusema wana nia ya
kuyapinga huku Jaji akisema anakubaliana na hoja zao na Agosti 4, 2017
maombi hayo ya dhamana yataanza kusikilizwa.
Katika
maombi hayo Yusuf Manji anaiomba Mahakama Kuu itengue hati ya kunyimwa
dhamana iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa kuwa ana
matatizo ya kiafya akisumbuliwa na matatizo ya moyo.
SHARE
No comments:
Post a Comment