Katibu
Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole
Gabriel (kushoto) akiongea na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Radio ya Efm
Bw. Francis Ciza wakati wa ziara yake kutembelea chombo hicho cha
habari jana Jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole
Gabriel akiongea na watumishi wa Radio ya Efm (hawapo katika picha)
alipofanya ziara ya kutembelea chombo hicho cha habari jana Jijini Dar es
Salaam.
Watumishi
wa Radio ya Efm wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni
Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (hayupo katika picha)
alipotembelea chombo hicho cha habari jana Jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole
Gabriel (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Radio ya
Efm pamoja na watendaji wa Wizara ya Habari wakati wa ziara yake jana
Jijini Dar es Salaam
Katibu
Mkuu Wizara Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole
Gabriel (kulia) akiongea na Viongozi wa Radio One na ITV alipofanya
ziara yake IPP Media Jijini Dar es Salaam kushoto kwake ni
Mkurugenzi Mtendaji Radio One na ITV Bi. Joyce Mhaville.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole
Gabriel (kushoto) akipata maelekezo kutoka kwa Mkurugenzi wa ITV/Capital
Tv Bw. Koigi Wacharia wakati wa ziara yake kutembelea Chombo hicho cha
Habari leo Jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole
Gabriel (aliyekaa) pamoja na watendaji wa Wizara ya Habari wakiangalia
namna mfumo wa urushwaji wa habari unavyofanya kazi katika studio za ITV
wakati wa ziara yake Jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole
Gabriel (aliyekaa kushoto ) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa
Radio One/ITV na watendaji wa Wizara ya Habari wakati wa ziara yake
leo Jijini Dar es Salaam.
Picha na: Genofeva Matemu – MAELEZO
…………………………
Na Lorietha Laurence-WHUSM
Serikali
imeeleza kuwa inathamini na kutambua mchango mkubwa unaotolewa na
Vyombo vya Habari nchini katika kuhakikisha kuwa jamii inapata taarifa
sahihi na kwa wakati.
Akizungumza
katika ziari yake alipotembelea vyombo vya habari vya Radio EFM na
Radio One/ ITV leo Jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel amesema kuwa lengo
kubwa la Serikali ni kuwepo kwa ushirikiano mzuri na sekta ya habari
nchini.
“Lengo
la ziara hii ni kuimarisha uhusiano baina ya Serikali na vyombo vya
habari pamoja na kufahamu utendaji wenu wa kazi na namna mnavyosimamia
maudhui ya vipindi vyenu mnavyoviandaa” amesema Prof. Gabriel
Aidha
aliongeza kuwa ni jambo jema linalofanywa na watanzania wazawa kuwekeza
katika sekta ya habari kwa kuwa dunia ya sasa imetawaliwa na utandawazi
kupitia taarifa mbalimbali zinazotolewa zenye lengo la kuhabarisha na
kujenga taifa letu.
Kwa
upande mwingine Prof. Gabriel amewataka watumishi wa vyombo hivyo vya
habari kufanya kazi kwa kuzingatia maadili, weledi na uzalendo ili
kufikia malengo waliyojiwekea.
Pia
amewataka watumishi wa vyombo hivyo vya habari kujenga utamaduni wa
kufanya kazi kwa kujituma ili kupata matokeo chanya katika soko la
ushindani na kuifikia jamii kubwa zaidi katika kutoa habari za uhakikia
na zenye usahihi.
Sambamba
na hilo Prof. Gabriel amevitaka vyombo hivyo vya habari kuzingatia
maudhui yanayoendana na jamii ya kitanzania pale wanapoandaa vipindi
mbalimbali ili kujenga jamii yenye utamaduni mzuri ikiwemo kufanya kazi
kimkakati.
Naye
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Redio Efm, Bw. Denis Ssebo amesema kuwa
uongozi wa radio yake upo tayari kufanya kazi kwa ukaribu zaidi na
Serikali lengo likiwa ni kuhakikisha wanafuata sheria na kanuni za
utangazaji ili kufanya kazi kwa kiwango chenye ubora .
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Radio One/ITV Bibi. Joyce Mhaville
ameishukuru serikali kupitia wizara ya Habari kwa kuonyesha ushirikiano
mzuri na vyombo vya habari ikiwemo kufanya kazi kwa karibu na
kuviwezesha vyombo hivyo kupata habari zenye ukweli na uhakika.
SHARE
No comments:
Post a Comment