TRA

TRA

Friday, July 28, 2017

Marekani kuiwekea vikwazo Urusi, Korea Kaskazini

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !



Bunge la Senate nchini Marekani limepiga kura ya kuziwekea vikwazo vipya Urusi, Iran na Korea Kaskazini licha ya pingamizi kutoka Ikulu ya White House.

Bunge la waakilishi liliidhinisha mswaada huo mapema wiki hii kwa kura nyingi. Baada ya mswaada huo kupita katika mabunge yote sasa utapelekwa kwa Rais Donald Trump kuwekwa sahihi.

 Trump anataka kuboresha uhusiano na Urusi

Lakini bwana Trump anataka kuboresha uhusiano na Urusi na anaweza kuukataa licha na uungwaji mkono uliopata.
Vikwazo hivyo ni vya kuiadhibu Urusi zaidi kufuatia hatua za kulimega eneo la Crimea kutoka Ukrain mwaka 2014.
Lakini mjadala kuhusu vikwazo hivyo vipya unafanyika huku uchunguzi kuhusu hatua za Urusi kuingilia kati uchaguzi wa Marekani wa mwaka 2016 ukiendelea.

Bwana Trump mara nyingi amekana kuwa Urusi iliingilia uchaguzi huo kusaidia kampeni yake.

Waandishi wa masuala ya siasa wanasema kuwa ikiwa Trump atajaribu kuukataa mswaada huo basi itakuwa ishara tosha kuwa anaiunga mkono sana Urusi.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger