Iran imefanikiwa
kuifanyia jaribio roketi ambayo ina uwezo wa kupeleka setilaiti hadi
mzingo wa dunia, siku moja baada ya Marekani kuiwekea vikwazo vipya
kufuatia mpango wake ya kinyuklia.
Ndilo jaribio la tano la roketi iliyoundwa nchini Iran tangu mwaka 2009. Televisheni ya taifa nchini Iran inasema kuwa roketi hiyo itabeba setilaiti ya uzito wa kilo 250 hadi umbali wa kilomita 500 angani.
- Iran yajaribu kombora la nyuklia
- Mwanazuoni wa Iran aachiliwa gerezani
- Iran yaitahadharisha Marekani kuhusu vikwazo
- Uwezo wa kijeshi wa Korea Kaskazini
Iran iliapa kujibu vikwazo vipya viivyotangazwa na Marekani ambavyo vililenga makampuni 18 au watu ambao wameunga mkono programu za Makombora za Iran.
Vikwazo hivyo vipya vilitangazwa siku moja baada ya utawala wa Trump kusema kuwa Iran inatekeleza makubaliano ya mwaka 2015 ya kuachana na mpango wa kinyukia.
Chanzo: BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment