Jumuiya
ya Waislam wa Ahmadiyya Kanda ya Ziwa (Ahmadiyya Muslim Jamaat Kanda ya Ziwa Julai 9,2017 imefanya mkutano wa mwaka wa Jumuiya
hiyo kwa mwaka 2017.
Mkutano
huo umefanyika katika Msikiti wa Ahmadiyya Muslim Jamaat Tz Masjid Fath
uliopo katika kijiji cha Sungamile kata ya Mwalugulu wilaya ya Kahama
mkoani Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga
Zainab Telack aliyekuwa ameambatana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na
usalama wa mkoa huo.
Akizungumza
wakati wa mkutano huo,Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya
Tanzania Maulana Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry alisema uislamu ni amani
hivyo lengo la mkutano huo ni kuhamasisha amani katika jamii kwa
kuwakumbusha waumini kumjua mwenyezi mungu.
Alisema
endapo jamii itakuwa na hofu ya mungu itasaidia kwa kiasi kikubwa
kupunguza hata kumaliza kabisa vitendo viovu katika jamii ikwemo mauaji
ya watu wasio na hatia kama vile vikongwe na watu wenye ualbino.
Katika
hatua nyingine Sheikh Chaudhry alisema Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya
ipo katika nchi 209 duniani ikiwemo Tanzania na mpaka sasa wamejenga
misikiti 25 katika mkoa wa Shinyanga na Simiyu.
“Jumuiya
hii imeingia Tanzania takribani miaka minne iliyopita,kupitia mikutano
yetu huwa tunaihamasisha jamii kuishi kwa amani,kufundisha watu watende
mambo mema lakini pia tunaweka umeme wa jua na kuchimba visima katika
vijiji ambavyo tumejenga misikiti yetu”,aliongeza.
Katibu
Mkuu Msaidizi wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Tanzania Abdulrahman
Mohammed Ame alisema sifa kuu ya uislam ni kuishi kwa amani na binadamu
wengine na wala siyo kutisha watu wengine.
Kwa
upande wake mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack alitumia fursa hiyo
kuwaomba viongozi wa dini kuendelea kuhamasisha amani katika jamii na
kutoa mafunzo kwa waumini wao kama wanavyotamka na si vinginevyo.
“Viongozi
wa dini mna jukumu la kuihamasisha jamii kuzuia makundi yasiyofaa
katika jamii,toeni mafunzo yenye kujenga jamii na watanzania muwe tayari
kutoa ushirikiano pale mnapoona kundi la watu flani wanataka kuleta
uvunjifu wa amani”,alieleza Telack.
Aidha
mkuu huyo wa mkoa aliipongeza Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya kwa
jitihada inazofanya katika kuhubiri amani katika jamii na kukemea
vitendo viovu ikiwemo kuua watu wasio wakiwemo wazee na watu wenye
ualbino pia kunyanyasa wanawake na watoto katika jamii.
SHARE
No comments:
Post a Comment