TRA

TRA

Monday, July 3, 2017

Mobisol inavyotoa huduma Maonesho ya Sabasaba

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !





Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa Kampuni ya Mobisol ya Ujerumani inayofunga umeme wa sola nchini, Leslie Katharina Otto, (kushoto) akitoa maelezo kwa mwananchi aliyetembelea banda la Mobisol Uwanja wa Maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar e Salaam. Kampuni hiyo pia imezindua TV inayotumia umeme wa jua nchini.
 
Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Mobisol kutoka Ujerumani ambayo inafunga na kuuza vifaa bora vya nishati ya umeme imezindua shughuli zake rasmi Jiji la Dar es Salaam pamoja na bidhaa mpya ya kipekee kwenye soko la Tanzania, ambayo ni TV ya sola inayojitegemea.

Akizungumza jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika hafla ya uzinduzi rasmi, kwenye banda la Ujerumani, katika viwanja vya sabasaba, Meneja Mkuu wa Mobisol Afrika Mashariki, Henrik Axelsson akiwa na mwakilishi wa Mobisol, Kanda ya Dar es Salaam, Allan Rwechungura, alisema Mobisol imesikia wito wa wakazi wa Dar es Salaam kutaka nishati nafuu, safi na salama na ndiyo maana imewekeza nguvu kubwa katika mkoa huo.

Kwa mujibu wa Henrik hiyo ni fursa nzuri ya wakazi wa Dar es Salaam kuchangamkia fursa ili kupata bidhaa hii mpya ambayo Mtanzania yeyote wa kawaida anaweza kumiliki. TV hii mpya ya kioo bapa yenye ubora wa hali ya juu ya sola inajitegemea na ina uwezo wa kuwasha taa na kuchaji simu hivyo ni ya kipekee na inajitegemea kwa upande wa nishati.

TV hiyo ya kisasa ya kioo bapa yenye ubora wa hali ya juu, ina betri inayofanya kazi hadi masaa 10, ina uwezo wa kuwasha taa, una waranti ya miaka mitatu na huduma baadaa ya mauzo.

Alisema katika msimu huu wa  Sabasaba kampuni ya Mobisol imetoa punguzo maalumu kwa ajili ya kuwawezesha watanzania wengi kuunganishwa na umeme wa sola wa uhakika ikiwemo kujipatia vifaa imara na vya kisasa vilivyotengenezwa kwa teknolojia ya Kijerumani kwa gharama nafuu na kuweza kulipia kwa awamu mpaka kufikia kipindi cha miaka mitatu.

"Ofa hii inawezesha wateja wetu watakaolipa fedha taslimu kuunganishwa na mtandao wa Mobisol kupata punguzo hadi asilimia 25%  na watakaolipia kwa awamu gharama ya kuanzia ni sh. 59,000 ambapo makato ya kila mwezi itakuwa sh. 33,500 ambapo kwa miaka mitatu itakuwa sh.1,266,000," alisema Rwechungura. 

Aliongeza kuwa kampuni ya Mobisol ina mitambo ya nguvu kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya nyumbani  ya wati 80, 120, na 200 mbayo inakuja pamoja na betri, taa, TV, redio, tochi na waya wa kuchaji simu hivyo kumwezesha mtu anayeishi eneo ambalo umeme haujafika kutokuwa na tofauti na mtu aishiye mjini.

Akibainisha zaidi uwezo wa kufanya kazi wa TV hii ya sola inayojitegemea ikitumika kwa TV, kuwasha taa 3 (za wati 1) kwa muda wa masaa 6 na kuchaji simu 2 unaweza kufanya kazi kati ya masaa 6 hadi 9.  Matumizi ya King’amuzi na kuwasha taa 3 kwa masaa 6 ya kuchaji simu 2 unaweza kufanya kazi kati ya saa tano na saba.

Rwechungura aliendelea kufafanua kuwa iwapo mteja atawasha TV kwa masaa 4 na kuchaji simu 2 ataweza kutumia taa kwa masaa 10 hadi 15.

"Mtambo huu wa Tv ya sola unaowezesha matumizi ya aina mbalimbali unapatikana kwa gharama ya sh. 950,000 na vifaa vya umeme ambayo mteja ataweza kununua na kutumia kwenye mtambo huu ni seti ya taa ya umeme yenye megawati moja au mbili, kifurushi cha king’amuzi cha zuku chenye chaneli za kulipia, redio ndogo na seti ya kuchaji simu. Hii ni fursa nyingine ya pekee kwa wateja kujiunga na familia ya Mobisol na kufurahia maisha ya kisasa kwa kutumia vifaa vya teknolojia bora kutoka Ujerumani," alisema.

Mobisol ni kampuni pekee katika kanda ya Afrika yenye mitambo ya kuzalisha umeme wa nishati ya jua wenye nguvu na inauza vifaa bora vya majumbani vya matumizi ya nishati ya umeme wa  jua ambapo pia imekuwa inatekeleza mpango wa kusambaza nishati ya umeme wa jua kwa kulipia kwa

Kufikia sasa inao mtandao wa wateja zaidi ya 62,000 nchini Tanzania na zaidi ya wateja 85,000 katika kanda ya nchi za Afrika Mashariki. Mobisol sasa ipo katika mikoa 23 nchini Tanzania na inalendelea kusogeza huduma karibu na wahitaji.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger