Mtoto wa kiume wa Rais wa Marekani, Donald Trump amevishambulia vyombo vya habari kufuatia
madai ya mkutano na wakili mrusi ambaye alisema kuwa alikuwa na habari
za kumchafulia jina Hillary Clinton.
Maafisa nchini Marekani wanachunguza madai yanayohusu Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani.
Mkwe wa Trump Jared Kushner na aliyekuwa mkuu wa kampeni Paul J Manafort, walikuwa pia katika mkutano huo na Natalia Veselnitskaya.
Trump Jr anasisitiza kuwa wakili huyo hakutoa taarifa muhimu kumhusu Bi Clinton, ambaye alikuwa mshindani wa babake katika kiti cha urais.
Mkutano huo ulifanyika tarehe 9 mwezi Juni mwaka 2016 katika jengo la Trump Tower, wiki mbili baada ya Donald Trump kupata uteuzi wa Republican.
Unaaminiwa kuwa mkutano wa kwanza wa siri kati ya raia wa Urusi na watu waliokuwa karibu na Trump.
Baada ya New York Times kuripoti mara ya kwanza kuhusu mkutano huo siku ya Jumamosi, Trump Jr alitoa taarifa iliyothibitisha kuwa mkutano huo ulifanyika lakini haikutaja ikiwa ulihusu kampeni ya kuwania urais.
CHANZO: BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment