Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi
Mkuu wa NIDA, Alphonce Malibiche akipokea tuzo toka kwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. John Magufuli
wakati wa sherehe za ufunguzi rasmi wa maonyesho ya 41 ya Kimataifa ya
Sabasaba yaliyofanyika hivi karibuni. NIDA ilikuwa mshindi wa kwanza
katika kundi la banda bora kwa Wizara na Taasisi za Serikali.
Mamlaka ya Vitambusho vya Taifa
(NIDA) imekuwa moja ya taasisi zilizofanya vizuri katika maonyesho ya
Sabasaba mwaka huu kwa kupata tuzo ya Banda Bora katika kundi la Wizara
za Serikali na Taasisi “Best Exhibitor Government Ministries &
Agencies” kwenye Maonesho ya Kimataifa ya 41 Sabasaba, yanayoendelea
katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa
Dar-es-salaam. Takribani kampuni za Ndani 2500 zikiwemo Wizara na
Taasisi za Serikali zinashiriki maonyesho hayo, pamoja na kampuni za
kigeni 500 zinazowakilisha Nchi 30 duniani.
Maonyesho hayo yaliyoanza tarehe
28 Juni 2017 yanatazamiwa kumalizika Julai 13, 2017. Mamlaka ya
Vitambulisho (NIDA) katika maonyesho ya mwaka huu imekuwa ikitoa huduma
mbalimbali kwa wananchi zinazohusu Utambuzi na Usajili wa Watu ikiwemo
huduma ya Usajili wa Vitambulisho vya Taifa na uchukuaji alama za
Kibailojia, kusaidia wananchi waliokwisha sajiliwa na hawajapata
vitambulisho vyao, kujua hatua za Maombi yao pamoja na kutoa Elimu kwa
umma kuhusu faida, umuhimu na matumizi mapana ya Kitambusho cha Taifa
katika ukuzaji Biashara na maendeleo ya Viwanda sambamba na kauli mbiu
ya Maonyesho hayo “Ukuzaji wa Biashara kwa maendeleo ya Viwanda.
NIDA imehakikisha ushiriki wao
katika Maadhimisho ya mwaka huu unaendana na kasi ya Serikali ya Awamu
ya Tano ya “Hapa Kazi Tu” kwa kuhakikisha wananchi wanaosajiliwa katika
siku 13 za maonyesho hayo wanapata Vitambulisho vyao ndani ya siku hizo.
SHARE
No comments:
Post a Comment