Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa
Mtwara Bw. Elias Nyabusami akifungua mafunzo yaWaganga Wakuu, Makatibu
wa Afya,Maafisa TEHAMA,Maafisa Mipango,Wahasibu na Wachumi kutoka
katika Mikoa ya Lindi,Mtwara, Ruvuma na Dar es Salaam kuhusu mfumo mpya
wa kuandaa Mipango na bajeti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa leo mjini
Mtwara.
Mkuu wa Timu ya Rasilimali Fedha
Kutoka mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma ujulikanao kwa
Kiingereza kama (Public Sector Systems Streghthen PS3.) unaofadhiliwa na
Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID) Bw. Gemini Mtei
akizungumza wakati wa mafunzo hayo leo Mjini Mtwara.
Afisa TEHAMA mwandamizi kutoka
Ofisi ya Rais TAMISEMI bw. Archibold Kundasai akitoa maelezo kwa
washiriki kuhusu faida za mfumo wa PS3 wakati wa hafla yaufunguzi wa
mafunzo hayo.
Mmoja wa watoa mada kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI bw. James Mtakatifikolo akiwasilisha mada katika mafunzo hayo.
Washiriki wa Mafunzo hayo wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasiishwa.
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa
Mtwara Bw. Elias Nyabusami (Katikati) akiwa na sehemu ya washiriki wa
mafunzo hayo kwenye picha ya pamoja mara baada ya kufungua mafunzo
hayo.
Meneja wa mradimradi wa
Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma ujulikanao kwa Kiingereza kama
(Public Sector Systems Streghthen PS3.) Mkoa wa Mtwara unaofadhiliwa na
Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID) Bw. Deosdedit
Msofe akizungumza wakati wa mafunzo hayo leo Mjini Mtwara.
Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo akizungumza wakati wa mafunzo hayo leo mjini Mtwara.
(Picha zote na Frank Mvungi- Maelezo Mtwara)
……………………..
Frank Mvungi Maelezo-Mtwara
Serikali kuokoa Kiwango Kikubwa
cha Fedha kutokana na kuanza kutumika kwa mfumo ulioboreshwa katika
kuandaa Mipango na Bajeti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa uitwao Plan
Rep unaoenda sambamba na mafunzo yanayoendeshwa kupitia mradi wa
Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma ujulikanao kwa Kiingereza kama
(Public Sector Systems Streghthen PS3.) unaofadhiliwa na Shirika la
Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID).
Akifungua mafunzo kwa
yaliyowashirikisha Waganga Wakuu, Makatibu wa Afya,Maafisa
TEHAMA,Maafisa Mipango,Wahasibu,Wachumi kutoka katika Mikoa ya
Lindi,Mtwara, Ruvuma na Dar es Salaam ,Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa
Mtwara Bw.Elias Nyabusami amesema mafunzo hayo yamekuja wakati muafaka
na yatasaidia kuondoa Changamoto zilizokuwa zikijitokeza kabla ya kuwepo
kwa mfumo huo.
‘’Kutokana na mabadiliko na
kurahisishwa kwa Teknolojia mfumo mpya wa Plan Rep umerahisihwa kwa
kufanywa kuwa web Based na utawezesha Halmashauri kuingiza taarifa za
mipango na bajeti moja kwa moja kwa njia ya mtandao na kuweza kutumwa
kwenye mfumo mmoja uliopo Ofisi ya Rais TAMISEMI ili kufanyiwa kazi na
kuingizwa kwenye bajeti Kuu ya mwaka husika”Alisisitiza Nyabusami
Akifafanua amesema kuwa mfumo huo
utasaidia kutoa mrejesho wa mara kwa mara kwa ngazi husika za utawala
kwa wakati na hakutakuwa tena na haja ya wahusika kusafiri kutoka
katika vituo vyao vya kazi ili kushughulikia masuala ya bajeti na
Mipango kwa kuwa sasa yatafanyika katika Mikoa na Halmashauri husika.
Kwa upande wake Mkuu wa Timu ya
Rasilimali Fedha Kutoka mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma
ujulikanao kwa Kiingereza kama (Public Sector Systems Streghthen PS3.)
Bw. Germini Mtei amesema kuwa kupitia mfumo mpya wa Plan Rep Mipango
yote na Bajeti za Vituo vya kutolea Huduma kwa wananchi itaonekana
kupitia mfumo huo hali itakayosaidia kuongeza ufanisi,uwazi ,
uwajibikaji na kuboreshwa kwa utoaji huduma.
“Kwa kutumia mfumo huu mpya sasa
tunaamini kuwa utasaidia kuondoa ucheleweshaji wa fedha kwenda kwenye
miradi na upotevu wa fedha kwa kuwa kila kitu kitafanyika kwa njia ya
mtandao” Alisisitiza Mtei.
Aliongeza kuwa mradi wa
Uimarishaji wa Mifumo ya sekta za Umma (PS3) unaotekelezwa katika mikoa
13 na Halmashauri 93 za Tanzania bara na PS3 inafanya kazi katika sekta
mbalimbali ikiwemo kuimarisha mifumo ya mawasiliano,Utawala Bora,Fedha
na rasilimali watu,husasani kwa jamii zenye uhitaji.
Aidha Afisa TEHAMA mwandamizi toka
Ofis ya Rais TAMISEMI Bw. Archibold Kundasai amesema kuwa mipango yote
kuanzia ngazi ya Kata,Halmashauri na Mikoa itakuwa katika mfumo huo na
dhamira ya Serikali ni kuongeza tija katika kuwahudumia Wananchi.
“Bajeti ilikuwa ikichukua muda
mrefu kuandaliwa ambapo takribani miezi 4 ilitumika ambapo kwa mfumo huu
tija itaongezeka kwa kuwa wahusika watabaki katika vituo vyao
wakihudumia wananchi huku wakitekeleza jukumu la Kuandaa Bajeti na
Mipango yao” Alisisitiza Kundasai
Naye Mshiriki wa Mafunzo hayo Bw.
Ezekiel Buyagaza ambaye ni Afisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya
Masasi amesema kuwa anaipongeza Serikali kwa maboresho yanayofanyika
hali itakayochochea tija katika kutoa huduma kwa wananchi.
Serikali ya Tanzania na USAID
kupitia mradi wa uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)imeandaa
mafunzo haya kwa watumiaji wake nchi nzima,Mafunzo yanatolewa na
Wakufunzi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI,Wakala ya Serikali mtandao,Ofisi
ya Rais Utumishi na Utawala Bora,Wizara ya Fedha na Mipango,Wizara ya
afya na unatarajiwa kutumiwa na watumiaji 1500 watakaofundishwa matumizi
ya mfumo huo.
SHARE
No comments:
Post a Comment