Mkuu
wa Wilaya ya Kilolo Asia Abdallah akizungumza na wanachama na wadau wa
timu ya lipuli kwenye mkutano wa uchaguzi wa kuwapata viongozi wapya wa
timu ya lipuli uliofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari ya
Mwembetogwa.
Baadhi ya wadau na wanachama wa timu ya lipuli wakiwa makini kumsikiliza mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Kilolo bi Asia Abdallah
Na fredy Mgunda, Iringa.
Mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah aliwataka wananchi wa Mkoa wa Iringa kuishi bila kuwa na majungu kwa sababu majungu yanarudisha nyuma maendeleo.
Na fredy Mgunda, Iringa.
Mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah aliwataka wananchi wa Mkoa wa Iringa kuishi bila kuwa na majungu kwa sababu majungu yanarudisha nyuma maendeleo.
Hayo
yamesemwa wakati wa hotuba ya uchaguzi wa kuwapa viongozi wapya wa timu
ya Lipuli katika ukumbi wa shule ya sekondari ya mwembetogwa ulipo
Manispaa ya Iringa.
Abdallah alisema
kuwa Iringa kumekuwa na majungu ambayo yamekuwa yakileta uchonganishi
baina ya watu na watu pia viongozi na viongozi hivyo inatakuwa
kubadilika na tusiishi kwa mazoea.
“Ukiiinga
huku majungu kule majungu hasa mtu hana pesa ya kula lakini anashinda
kwenye mitandao ya kijamii kuleta majungu,fanyeni kazi kwa nguvu zenu
zote maana mnaendekeza tu majungu ambayo hayana manufaa kwako binafsi
hata taifa kwa ujumla”alisema Abdallah
Aidha Abdallah alisema
kuwa viongozi wa timu ya lipuli watakaoingia madarakani kuhakikisha
wanavunga makundi yote ya majungu na kuhakikisha timu inakuwa na umoja
na ushirikiano kila nyanja ili kupata mafanikio makubwa ambaya yataleta
faraja kwa wakazi wa Iringa na wapenda Soka.
“Haiwezikani
kila kona ni majungu tu hivi nyie hamna kazi za kufanya tena afadhali
wanawake wangekuwa na majungu lakini majungu hayo yanaongozwa na wanaume
kwenye magroup ya what’s up,achaneni na magroup ambayo hayana faida
kwako wala hanaya afya kwa taifa la Tanzania” alisema Abdallah
Mohammed
aliongeza kwa kusema kuwa Rais wa jamhuli ya muungano wa Tanzania Dr
John pombe Magufuli anahimiza wananchi kufanya kazi na sio kutengeneza
majungu ambayo yamekuwa yakikwamisha maendeleo ya wananchi.
Kwa
upande wake Katibu wa chama cha Soka Mkoani Iringa Dr Ally Ngalla
alimshukuru Mkuu wa wilaya huyo kwa hotuba nzuri na kumuahidi kuwa
Iringa itabadilika na kufuta majungu kutokana na tayari wamepata
viongozi wapya wa timu ya lipuli.
“Nikiwa
kama kiongozi nitahakikisha makundi yote ya majungu yanavunjwa na kuwa
kitu kimoja ambapo tutafanya kazi kama siafu ili kuinua Mpira wa miguu
Mkoani Iringa “alisema Ngalla
Ngalla
aliwata wadau wa mpira miguu Mkoani Iringa kusahau yaliyopita na
kuangalia nini cha kufanya ili kuisadia timu ya lipuli ifanye vizuri
kwenye ligi kuu Tanzania bara na kulejesha furaha ya wananchi wa Iringa.
Naye
Mwenyekiti Mpya wa timu ya lipuli Ramadhani Mahano aliwaomba wadau wa
Mpira na wapenzi wa timu ya lipuli kufanya kazi kwa ushirikiano pamoja
kuvunja makundi yote yaliyokuwa yanasababisha migogoro ya lipuli na
Mpira wa miguu kwa ujumla.
Nawaombeni
sana kuyaka kichwani vizuri maneno ya Mkuu wa Wilaya ya Kilolo bi
Asia Abdallah kwa kuacha majungu au kusababisha migogoro ambayo haina
maana bali naomba tushauriane kwa kila jambo kwa manufaa ya lipuli na
wadau wa mpira.
SHARE
No comments:
Post a Comment