TRA

TRA

Thursday, July 27, 2017

RAIS MAGUFULI AMVAA MBUNGE WA CCM MOROGORO.. AMTAKA ARUDISHE VIWANDA

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !

SeeBait

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli amembadilikia Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini, Aziz Abood na kumtaka arudishe viwanda mbalimbali ambavyo alibinafsishiwa na serikali kama ameshindwa kuviendesha.

Rais Magufuli amesema hayo leo alipokuwa Morogoro mjini na kuwataka watu waliobinafsishiwa viwanda na serikali mkoani humo na wameshindwa kuviendesha wavirudishe kwa serikali ili serikali iweze kuwapa watu wengine ambao wataweza kuviendesha.

“Ninarudia wito wangu niliokwisha kuutoa huko nyuma, kwamba wenye viwanda hapa Morogoro ambao wameshindwa kuviendesha, na leo nataja akiwemo Mbunge wa hapa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), narudia akiwemo Mbunge wa hapa wa CCM ambaye alibinafsishiwa viwanda vingi, kama ameshindwa kuviendesha avirudishe ili tuwape watu wengine kwa sababu vijana hawa wanakosa ajira, nazungumza kwa uwazi kwa sababu msema kweli ni mpenzi wa Mungu," alisisitiza Rais Magufuli.

Mbali na hilo Rais Magufuli amemuagiza Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro SACP - Ulrich Onesphory Matei kuhakikisha askari Mgambo hawawasumbuli wafanyabiashara wadogo wadogo na amewataka wafanyabiashara hao kutofanya vurugu wakati utaratibu mzuri unaandaliwa kwa ajili yao.

Rais Magufuli wakati akiwa katika ziara mkoani Singida aliweka wazi kuwa yeye anauchukia sana ubinafsishaji na kusema ndiyo umeturudisha nyuma na kuharibu mipango mizuri ambayo alikuwa nayo Mwalimu Nyerere, huku akitolea mfano viwanda kadhaa ambavyo vipo Morogoro na vimeshindwa kuendelezwa na majengo yake kugeuka magodauni ya watu.

==>>Hii ni taarifa ya Ikulu

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger