TRA

TRA

Thursday, July 27, 2017

Wanawake watano wachomwa moto hadi kufa Tabora

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Watu watano wameuwawa kwa kuchomwa moto katika kata ya Uchama Wilayani Nzega Mkoani Tabora na watu wanaosaidikiwa kuwa ni Sungusungu huku wakidaiwa wameuliwa kutokana na imani za kishirikina.

Kutokana na mauaji hayo Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri, amezitaka Kamati za Ulinzi na usalama ngazi ya Mkoa na ile ya Wilaya ya Nzega kusitisha shughuli zote zilizokuwa zikifanywa na sungusungu katika kijiji hicho.

Mwanri alisema kuwa amechukua hatua hiyo baada ya sungusungu hao kutekeleza mauaji hayo ya watu watano ambao wote ni wanawake wakituhumiwa kuwa ni washirikina.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Wilbroad Mutafungwa alisema katika kuendelea kuchunguza tukio hilo jeshi hilo linawashikilia baadhi ya viongozi wa kijiji hicho ili kuweza kubaini waliotekeleza tukio hilo.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger