Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony
Mtaka akizungumza na wadau wa Ushirika wa Mkoa huo(hawapo pichani)
wakati wa Uzinduzi wa Jukwaa la Ushirika la Mkoa huo Mjini Bariadi,
(kushoto) ni Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony
Mtaka(kushoto) akiteta jambo na Kaimu Naibu Mrajis kutoka Tume ya
Maendeleo ya Ushirika, Ndg.Collins Nyakunga wakati wa Uzinduzi wa Jukwaa
la Ushirika la mkoa wa Simiyu, Mjini Bariadi
Baadhi ya Wadau wa Ushirika Mkoa
wa Simiyu wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa mara baada ya
uzinduzi wa Jukwaa la Ushirika la Mkoa huo Mjini Bariadi.
Baadhi ya Wadau wa Ushirika Mkoa
wa Simiyu wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa mara baada ya
uzinduzi wa Jukwaa la Ushirika la Mkoa huo Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony
Mtaka akizungumza na wadau wa Ushirika wa mkoa huo (hawapo pichani)
wakati wa Uzinduzi wa Jukwaa la Ushirika la Mkoa huo Mjini Bariadi.
Afisa Ushirika Mkuu kutoka Tume ya
Maendeleo ya Ushirika Sehemu ya Uhamasishaji na utaratibu, Veneranda
Mgoba akiwasilisha mada ya Usimamizi na Udhibiti kwa wadau wa Ushirika
wa Mkoa huo(hawapo pichani) wakati wa Uzinduzi wa Jukwaa la Ushirika la
Mkoa huo Mjini Bariadi.
Mwanasheria kutoka Tume ya
Maendeleo ya ushirika Kitengo cha Sheria, Donald Deogratius
akiwasilisha mada ya Sheria ya Ushirika kwa wadau wa Ushirika wa Mkoa
huo(hawapo pichani) wakati wa Uzinduzi wa Jukwaa la Ushirika la Mkoa huo
Mjini Bariadi.
………………………………
Na Stella Kalinga, Simiyu
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka amesema Mkoa huo unahitaji ushirika imara na wa kisasa
unaolenga kuwafikisha wananchi katika Uchumi wa kati.
Mtaka amesema hayo wakati wa
uzinduzi wa Jukwaa la Ushirika la Mkoa wa Simiyu uliofanyika katika
Ukumbi wa kanisa Katoliki Mjini Bariadi, tukio ambalo limeshirikisha
viongozi Serikali na watalaam mbalimbali ngazi ya Mkoa na Wilaya,
viongozi wa vyama vya ushirika, Tume ya maendeleo ya Ushirika na wadau
mbalimbali wa ushirika.
” Sisi kama mkoa tuko tayari kwa
yale ambayo ninyi wenzetu wa Tume ya Ushirika mnadhani kupitia hayo
tutakuwa na ushirika imara na utakaoendeshwa kisasa, tuko tayari hata
kwa kuwatoa watu wetu kujifunza katika vyama vya ushirika
vilivyofanikiwa;ushirika wa Tanzania ukiamua Uchumi wa kati inawezekana”
Aidha, Mtaka amesema wananchi
wakielimishwa na kukubali kuungana katika vyama ushirika wanaweza
kuondokana na Umaskini, hivyo amesisitiza uwepo wa ushirika imara wenye
matokeo chanya katika maeneo muhimu ya uzalishaji, ili hata mikoa
mingine ijifunze Simiyu
“Mwalimu Nyerere amewahi kusema
namna pekee ya watu maskini kujikomboa ni kuungana, niwasihi
wanaushirika kuunganisha nguvu katika ushirika, matajiri wanaungana
kuunda makampuni yanayoweza kukopa, yakashtaki na kushtakiwa ninyi
unganeni kwenye vyama vya ushirika kujenga uchumi ” amesema Mtaka.
Aidha, Mtaka amesema Benki ya
Maendeleo ya Kilimo(TADB) imekubali kufanya kazi na Mkoa wa Simiyu kwa
kuviwezesha vyama vya ushirika na vikundi vilivyosajiliwa kisheria kwa
kuwajengea uwezo wanachama na kuwapa mikopo kwa ajili ya kuendesha
miradi mbalimbali, hivyo vyama vya ushirika vinapaswa kuchangamkia fursa
hiyo.
Akizungumzia mchango wa ushirika
katika utekelezaji wa Kauli Mbiu ya Mkoa”Wilaya Moja Bidhaa Moja Kiwanda
Kimoja” Mkuu huyo wa Mkoa amesema vyama vya ushirika ndivyo vyenye
wazalishaji wa malighafi ya viwanda, hivyo jukwaa la ushirika litumiwe
vizuri katika kuweka mikakati ya kuimarisha vyama vya ushirika na
Viongozi wa Serikali wako tayari kuonesha ushirikiano.
Katika hatua nyingine Mtaka
amesema mkoa unaandaa andiko linalolenga kuwakusanya wakulima na
wanaushirika wote pamoja, ambapo watatumia vyumba vya madarasa katika
Shule za Serikali wanafunzi watakapokuwa likizo kupewa mafunzo ya
ushirika na kilimo na Wataalam wa Halmashauri, Mkoa na Chuo Kikuu cha
Ushirika, ili kuimarisha ushirika na kuongeza tija katika kilimo na
mifugo.
Sanjali na hilo Mtaka amesisitiza
kuwa mkoa wa Simiyu ndio unaoongoza kwa kulima pamba hapa nchini, hivyo
ni vema kukawa na ushirika wenye kuleta majawabu kwa changamoto
zinazowakabili wakulima wa pamba kuondoa kero kwa wakulima na kuongeza
ubora katika uzalishaji.
Kwa Upande wake Kaimu Naibu Mrajis
kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika, Ndg.Collins Nyakunga amemshukuru
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu kwa kuonesha nia ya kuimarisha ushirika katika
mkoa huo na kuona kuwa kupitia ushirika wananchi wanyonge wanaweza
kutatua matatizo yao ya kiuchumi na Kijamii.
Nyakunga amesema Tume ya Maendeleo
ya Ushirika itaandaa namna ambayo itautoa ushirika katika uendeshaji wa
kizamani uendeshwe kisasa, tafiti zitafanyika kupitia Chuo Kikuu cha
Ushirika kuona namna ya kuongeza bei, thamani ya zao la pamba na
ushirika mkoani Simiyu kuimarika.
Naye Mrajis Msaidizi wa Vyama vya
Ushirika Mkoa wa Simiyu, Ndg Mathias Shineneko amesema Mkoa huo
umejiwekea mkakati wa kuakikisha vyama vya ushirika vinajielekeza katika
kuweka taratibu za kuongeza na kuimarisha mitaji, hisa na akiba ili
kujiimarisha kiuchumi.
Wakati huo huo Ezekiel Ganji
kutoka Chama cha Msingi Sola wilayani Maswa ameiomba Serikali
kuwashirikisha wakulima wa pamba katika maamuzi ya kupanga bei badala ya
kupangwa na makampuni yanayonunua pamba na kusisitiza kuwa katika
ukaguzi wa vyama vya ushirika Serikali iangalie uwezo wa vyama hivyo na
kupunguza tozo za ukaguzi kwa kuwa vyama vingi havina uwezo mzuri
kifedha.
SHARE
No comments:
Post a Comment