Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu
wenye ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama, (kulia), akizungumza Julai 27, 2017 wakati alipofanya
ziara ya ukaguzi wa kushtukiza kwenye Hospitali ya K’s iliyoko eneo la Mafyati
jijini Mbeya ili kubaini kama mwajiri kwenye hospitali hiyo amejisajili katika Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF). Waziri ametoa siku 30 kwa waajiri kutoka sekta ya
umma na binafsi Tanzania Bara, kujisajili na Mfuko huo, vinginevyo watakabiliwa
na adhabu mbalimbali ikiwemo faini ya shilingi milioni 50, kifungo cha miaka 5
jela au vyote kwa pamoja. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Afya na Tathmini
wa Mfuko huo, Dkt. Abdusalaam Omar.
NA MWANDISHI WETU MBEYA
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama,
ametoa siku 30 kwa waajiri wote nchini ambao hawajasajili, kujisajili katika
Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi (WCF), na kutoa michango kwa wakati, vinginevyo hatua
kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Waziri Mhagama alitoa agizo hilo jijini
Mbeya Julai 27, 2017 wakati wa zoezi la ukaguzi wa kushtukiza jijini
humo kuwabaini waajiri ambao bado hawajatekeleza Sheria ya Fidia kwa
Wafanyakazi Sura 263 Marejeo ya Mwaka 2015 kifungu cha 5, ambayo inawataka
waajiri wote kutoka sekta ya Umma na Binafsi, Tanzania Bara kujisajili kwenye
Mfuko huo.
“Mwajiri ambaye
hajajisajili kwenye Mfuko,
anaweza kufikishwa mahakamani na adhabu ni pamoja na kutozwa faini ya
kiasi cha
fedha kisichozidi shilingi milioni 50 au kifungo kisichozidi miaka 5
jela au
vyote kwa pamoja, hivyo nawasihi waajiri kutoka sekta binafsi na umma
Tanzania Bara ambao hawajasajili kutekeleza sheria hiyo inayowataka
kujisajili WCF
katika muda huo nilioutoa.” Alisisitiza Mhe. Waziri Jenista Mhagama.
Katika ziara hiyo ya ukaguzi wa
kushtukiza Mhe. Waziri alifuatana na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na
Tathmini wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omar, Mkuu
wa Kitengo cha Uhusiano cha Mfuko huo, Bi. Laura Kunenge na Afisa Kazi wa Mkoa
wa Mbeya, Bi. Mary Patrick Mwansisya ambapo taasisi ya kwanza ambayo Mhe. Mhagama
aliikagua ni Hospitali ya K’s iliyoko eneo la Mafyati na St. Aggrey iliyoko
Uyole na kubaini kuwa taasisi hizo hazijajisajili katika Mfuko.
Aidha Waziri alitoa siku saba kwa waajiri wote
Mkoani Mbeya wapatao 107 ambao bado hawajajisajili ikiwemo Hospitali ya K’s na
Shule ya sekondari St. Aggrey kujisajili ndani ya muda huo.
“Mkishindwa kutekeleza agizo hilo maana yake mnatuelekeza kutumia kifungu cha 71(4), cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi kinachotamka adhabu ya faini ya kiasi cha fedha kisichopungua shilingi milioni 50, kifungo cha miaka 5 jela au vyote kwa pamoja.” Alisema.
Aidha Waziri Jenista alihimiza kuwa
mwajiri anapojisajili na Mfuko pia atimize wajibu wa kisheria wa kuchangia
katika Mfuko kwa wakati stahiki. Mhe. Waziri alisema nia ya Serikali ya awamu
ya Tano sio kuwatisha waajiri bali ni kuhakikisha wanafuata sheria ili
hatimaye, wafanyakazi wapate haki yao stahiki pindi wanapoumia, kuugua ama
kufariki wakati wakiwa wanatekeleza majukumu ya mwajiri wao kwa mujibu wa
mkataba wa ajira.
Akifafanua zaidi Waziri alisema,
takwimu zilizopo katika Mfuko za kipindi cha mwaka 2015/16 na 2016/17
zinaonesha kuna jumla ya waajiri 229 jijini Mbeya na kati yao ni waajiri 107 tu
ndiyo waliojisajili katika Mfuko.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Afya na Tathmini wa WCF, Dk. Abdulsalaam Omar alisema Mfuko
unamshukuru Mhe. Waziri kwa kushiriki katika ukaguzi huu wa kwanza wa aina yake
kufanyika tangu Mfuko huu uanzishwe mnamo mwaka 2015 na kwamba Mfuko utasimamia
na kutekeleza maagizo ya Mhe. Waziri.
"Kwa kipindi chote hicho Mfuko
umekuwa ukijikita zaidi katika kutoa elimu kwa wadau mbalimbali wakiwemo
waajiri ili waweze kuelewa umuhimu wa kujisajili katika Mfuko na faida ambazo
mwajiri na mfanyakazi atazipata pindi anapoumia, kuugua au kufariki wakati
akitekeleza majukumu ya mwajiri,” alisisitiza Dkt Omar.
Akifafanua zaidi, Mkurugenzi huyo alisema
katika kazi ya uelimishaji kwa kipindi cha mwaka 2016/2017 Mfuko ulitoa elimu
kwa waajiri wapatao 4,901 kuhusu haki na wajibu lakini pia kuelewa sheria
kuhusu wajibu wa waajiri kujisajili katika Mfuko. Aidha Mfuko umekuwa ukitumia
njia mbalimbali kama vile vyombo vya habari, semina lakini pia kwa kuwaandikia
waajiri kuhusu umuhimu wa wao kutekeleza sheria hiyo kwa kujisajili katika
Mfuko na kutoa Michango kwa wakati kama ambavyo sheria inaelekeza.
Dkt Omar alisema Mfuko ulianza kutekeleza
majukumu yake tarehe 1 Julai 2015 kama ilivyoelekezwa katika tangazo la Serikali Na.
169/2015 ambapo majukumu hayo ni pamoja na kusajili waajiri, kukusanya michango
na kulipa fidia stahiki.
Tayari Mfuko umeanza kulipa fidia kwa
wafanyakazi walioumia, kuugua ama kufariki kuanzia tarehe 1 Julai 2016.
Ili mfanyakazi aweze kulipwa fidia, ni
lazima mwajiri wake awe amechangia katika Mfuko, hivyo waajiri wanao wajibu
kisheria chini ya Vifungu vya 71 – 78 vya Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi
kujisajili, kuwasilisha michango, kutoa taarifa ya matukio ya ajali na magonjwa
yatokanayo na kazi pamoja na kuwasilisha mapato ya mwaka." Alifafanua Dkt.
Omar.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano cha
Mfuko huo, Bi. Laura Kunenge alisema, "Tamko alilotoa Mhe. Waziri wetu
litakuwa chachu kwa waajiri wengine nchini kujiunga na Mfuko kwa kujisajili na kuwasilisha
michango kwa wakati na hivyo kuwezesha kufikia lengo la Mfuko la kulipa Fidia
Stahiki kwa wakati." Alisema.
Bi. Kunenge pia alisema,
Ofisi za WCF ziko wazi na kwamba huduma za Mfuko huo zinapatikana kila
mkoa hapa Tanzania Bara ambapo Maafisa Kazi wa Mikoa ndio wanafanya kazi
kwa niaba ya Mfuko kwa sasa.
Mkuu wa Kitengo cha
Uhusiano cha
Mfuko huo, Bi. Laura Kunenge. (kushoto), na Afisa Kazi Mkoa wa Mbeya,
Bi.Mary Patrick Mwansisya, (kulia), wakiuliza alipo mkurugenzi wa
Hospitali ya K's mara baada ya kuwasili na waziri Mhagama katika ziara
ya ukaguzi wa kushtukiza leo Julai 27, 2017.
Waziri Mhagama, (wakwanza kulia), Bi.
Laura na Dkt. Omar, wakimsubiri Mfanyakazi huyu wa K's Hospital
akiwasiliana kwa simu na mwajiri wake ili kumjulisha uwepo wa Waziri na
ujumbe wake kwenye hospitali hiyo.
Maafisa wa polisi wakiwa tayari kuhakikisha usalama unazingatiwa wakati wa zoezi hilo.
Waziri Mhagama na Dkt. Omar(kushoto), wakisubiri ujio wa Mkurugenzi wa hospitali ya K's
Afisa Matekeelzo Mwandamizi wa WCF,
Bw.Dan Kapogo, (kulia), akijadiliana jambo na Afisa Kazi Mkoa wa Mbeya,
Bi.Mary Patrick Mwansisya.
Mkuu
wa Kitengo cha Uhusiano cha
Mfuko huo, Bi. Laura Kunenge. (kushoto), Afisa Matekelezo Mwandamizi wa
Mfuko huo Bw. Dan Kapogo,na Afisa Kazi Mkoa wa Mbeya, Bi.Mary Patrick
Mwansisya, wakijadiliana jambo.
Mhe. Mhagama akisalimiana na Mkurugenzi
wa Hospitali ya K's Dkt.Victoria Kanama, baada ya kuitwa ili aonane na
waziri kueleza kwa nini hajajisajili na Mfuko licha ya kupatiwa elimu
lakini pia kujulishwa kwa barua.
Dkt. Omar, Kulia), akimuongoza waziri
Mhagama wakati wakitoka kwenye Hospitali ya K's baada ya ukaguzi.
(wakwazna kushoto) ni Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Dkt.Victoria Kanama.
Dkt. Omar akitoa shukrani za WCF
kufuatia ziara hiyo ya kushtukiza aliyofanya Mhe. Waziri na kubainisha
kuwa maagizo hayo yatasimamiwa na kutekelezwa.
Bi. Kunenge na Bw. Kapogo kutoka WCF wakijadiliana jambo
Mratibu wa Hospitali ya K's Bw.Mtunda Mwankwasya akizungumza.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano cha
Mfuko huo, Bi. Laura Kunenge
Afisa Kazi Mkoa wa Mbeya, Bi.Mary
Patrick Mwansisya akizungumza. "Tumewapa taarifa waajiri wote mkoani
Mbeya hivyo wanajua fika kuhusu sheria hii inayowataka kujisajili na
kutoa Michango katika Mfuko.
Dkt. Omar akiteta jambo na Mhe. Waziri Mhagama.
Waziri akitoka kwenye Hospitali ya K's akiongozana na Mratibu wa hospitali hiyo,Bw.Mtunda Mwankwasya
Mkuu wa shule ya St. Aggrey.
Waziri Mhagama akizungumza mbele ya Meneja wa shule ya St. Aggrey, Bw.Melas Paul Mdemu
SHARE
No comments:
Post a Comment