Na Regina Mkonde
Mbunge
wa Kigoma Mjini ambaye pia ni Kiongozi Mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo,
Zitto Kabwe amewajibu baadhi ya watu wanaomkosoa na kumuita msaliti
kutokana na kitendo cha kumsifia Rais John Magufuli alipokuwa ziarani
jimboni humo.
Zitto
alijibu mapigo hayo jana wakati akizungumza na wananchi wa Kigoma
Mjini, ambapo alisema asingeweza kumkosoa Rais Magufuli wakati ule kwa
kuwa alikuwa mgeni jimboni kwake, pia alikuwa anafanya shughuli za
maendeleo ya wananchi wa jimboni kwake.
“Rais
alikuja hapa akafungua mradi wa maji tukaenda ziwa Tanganyika, kuna
watu walikasirika sababu Rais alinisifia sana, hawezi akaja Kigoma mtu
akanisema mimi vibaya msingekubali, na mgeni akija siwezi nikaanza
kumsema vibaya, mgeni akija unamkaribisha anafanya kazi yake anaondoka,
kwani rais akienda kwenye majimbo yao wanamsema, rais alikwenda Bukoba
Mjini wakati wa tetemeko, mbunge wa jimbo hilo alimsema ? alikwenda
Arumeru kwa mdogo wangu Joshua Nasari, alimsema rais kwa nini akija
kigoma mimi ndio nimseme,” alihoji Zitto.
Aliongeza kuwa “Mimi
hamkunifundisha kuwa mazwazwa wazee mlinifundisha adabu na kuhakikisha
maendeleo yanapatikana lakini sio kwamba rais akikosea hatutamsema
tutamsema, na tumeshamsema sana, sisi ndio chama cha mwisho kufanya
mkutano wa ziara, tukaja operesheni ya linda demokrasia tumemaliza
mikutano ikapigwa marufuku.”
SHARE
No comments:
Post a Comment