Zuwema Mohammed ‘Shilole.
MWANAM-UZIKI
wa miondoko ya mduara, Zuwema Mohammed ‘Shilole’ ameweka wazi kuwa
huenda akaukacha muziki siku za usoni kutokana na kunogewa na biashara
yake ya kuuza chakula katika mgahawa wake.Akizungumza na Risasi Vibes,
Shilole alisema anaona biashara yake hiyo inampa faida nyingi kuliko
uigizaji na hata muziki anaofanya, hivyo kutokana na maisha magumu ni
bora kufanya kitu kinachomu-ingizia kipato.
“Huku kwa
mama ntilie naona kunanilipa zaidi ya sehemu nyingine ambazo nipo, sasa
ni bora kufanya kitu ambacho kina kuingizia kipato kuliko kung’ang’ania
sehemu ambayo haikulipi au inakulipa kidogo tena kwa kusubiri,” alisema
Shilole.
Stori: Imelda Mtema
SHARE
No comments:
Post a Comment