Soko hilo la City Market lililo mjini Lusaka, limekuwa likiteketea tangu mapema leo Jumanne.
Msemaji wa polisi Esther Katongo na meya wa mji wa Lusaka Wilson Kalumba wanasema kuwa bado wanachunguza chanzo cha moto huo.
Kisa hicho kimewaacha wafanybiashara wengi na majonzi baada kupoteza mali yao.
"Nitailisha vipi familia yangu kwa sabaua niliwa ninategemea hapa,?" alisema Loveness Banda huku akiangalia kutoka mbali soko likiteketea.
Walioshuhudia wanashuku kuwa moto huo ulisababishwa na hitilafu ya umeme na kuwalaumu wazima moto kwa kuchelewa kufika kuzuia moto huo kusambaa.
Soko hilo lina wafanyabiashara wengi zaidi nchini Zambia. Kati ya bidhaa zinazouuzwa ni pomoja na nguo za mitumba, vifaa vya elektroniki na hata chakula.
CHANZO: BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment