Bunge nchini
Tanzania limepitisha sheria mbili muhimu za uchimbani madini ambazo zina
lengo la kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya madini.
Kupitia sheria hizo sasa serikali ina matumaini kuwa wananchi watanufaika kutokana na mali asili ya nchi hiyo.
Moja ya sheria hizo inasema kuwa watu nchini Tanzania watakuwa na uhuru wa kudumu kwa mali yao ya asili na serikali kwa niaba ya watu itasimamia mali hiyo.
Hadi sasa sheria haikuweza kueleza wasi ni nani ana uhuru wa kusimamia mali asili ya nchi ya Tanzania.
- Mambo muhimu kuhusu sakata ya madini Tanzania
- Wajumbe wa kamati maalum ya madini Tanzania wateuliwa
- Madini mapya yagunduliwa Tanzania
- Magufuli amfuta kazi waziri wa nishati
Serikali inalaumu kampuni ya Acacia kwa kutofichua kiwango cha madini inachopeleka nje ya nchi na kukosa kulipa kodi ya mamilioni ya dola kwa muda wa miaka 20 imekuwa ikihudumu nchini humo.
Kampuni hiyo hata hivyo imepinga takwimu hizo za serikali ikisema kuwa ikiwa zilikuwa za ukweli, basi Tanzania ingekuwa mzalishaji mkubwa zaidi wa dhahabu na shaba duniani.
SHARE
No comments:
Post a Comment