Na Humphrey Shao ,Globu ya Jamii.
Kampuni
inayoongoza kwa utoaji wa huduma bora na nafuu za matangazo ya dijitali
nchini ya StarTimes, imetangaza kushusha ofa ya Ving'amuzi katika
Maonyesho ya 41 ya Sabasaba inawatangazia wateja wake na watanzania kwa
ujumla kutembelea banda
lao.
Akizungumza
na Globu ya Jamii Meneja Mauzo wa Star Times Tanzania amesema kampuni
hiyo inawapa wateja ving’amuzi vya bei rahisi vilivyounganishwa na
kifurushi cha bure kwa mwezi moja vinapatikana
kwa shilingi 78,000 kwa dishi na 47000
kwa antena.
amesmea kuwa pia
wateja wataweza kununua televisheni ya kidigitali kwa bei nafuu zaidi na kupewa
punguzo la asilimia 8% ambapo kutakuwa na inchi 40,32 na 24 yenye
kingamuzi ndani yake na kukupa chaneli zaidi ya 100 za kitaifa na kimataifa ili
kufurahia ulimwengu wa kidigitali .
"Mbali
na hayo,kutakuwa na bidhaa nyingine kama simu za kisasa na projekta ambazo zinapatikana
kwa bei nafuu ambayo kila mtanzania anaweza kumudu.
Lengo
la kufanya hivi ni kumuwezesha kila mtanzania aweze kumudu gharama za matangazo
na kufurahia ulimwengu wa kidijitali.
Pia
tungependa kuwahamasisha wateja wetu kulipia vifurushi tulivyonavyo ili kuweza
kutazama chaneli na vipindi vingi zaidi tulivyonavyo vya kitaifa na kimataifa." Amesema Kisaka.
Amesema kuwa wateja wa StarTimes wanafurahia matangazo ya moja kwa moja ya kombe la mabara,
Mwezi ujao tutaanza kuonyesha kombe la mabingwa kimataifa ( ICC),ligi kuu ya
ujerumani (Bundersliga),ligi kuu Italia (Serie A), ligi kuu Ufaransa (League 1)
na mwakani kombe la dunia litakalofanyika nchini Urusi.
Tunazo
tamthiliya, filamu za kiafrika na ulaya, kichina kihindi, vipindi vya watoto na
kadhalika.Vilevile utaweza kuangalia chaneli zaidi ya 37 mubashara na Bure
kupitia APP yetu inayopatikana kupitia Google store, App store au
www.startimestv.com.
SHARE
No comments:
Post a Comment