MKUU wa Wilaya Kibaha, mkoani Pwani, Asumpter
Mshama, amewapongeza washindi wa Bahati Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’ na
kuwataka kuweka umakini na malengo katika fedha zao wanazokabidhiwa ili
wanufaike kiuchumi.
Meneja
Masoko wa Bahati Nasibu ya Biko, Goodhope Heaven kushoto akimuelekeza
jambo Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Asumpter Mshama katikati
wakati wa kumkabidhi mshindi wa Sh Milioni 20 wa droo ya 19 ya Biko,
Elisiana Laizer kulia mwenye gauni jekundu ndani ya Benki ya NMB, Tawi
la Mlandizi, wilayani Kibaha, mkoani Pwani.
DC Asumpter ameyasema hayo jana katika tawi la NMB, Mlandizi,
Wilayani Kibaha, mkoani Pwani katika makabidhiano ya Sh Milioni 20
zilizokabidhiwa kwa Mshindi wa droo ya 19, Elisiana Simon Laizer, mjasiriamali
wa kutengeneza sabuni, mwenye maskani yake Mlandizi, aliyeibuka kidedea katika
droo ya 19 ya bahati nasibu hiyo ya aina yake inayochezwa kwa njia ya ujumbe
mfupi wa maandishi kwa simu za mikononi za Tigo, Vodacom na Airtel.
Akizungumzia bahati nasibu hiyo ya Biko, DC Mshama alisema
michezo ya kubahatisha ina nafasi kubwa ya kukuza uchumi wao na uchumi wa Taifa
kwa kuhakikisha kwamba wanafanya shughuli zenye kuleta maendeleo badala ya
kuzitumia kwa mambo yasiyokuwa na msingi.
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha,
Mheshimiwa Asumpter Mshama kulia akimkabidhi jumlaa ya Sh Milioni 20,
mshindi wa Biko droo ya 19, mjasiriamali wa kutengeneza sabuni, Elisiana
Laizer, mwenye maskani yake Mlandizi, wilayani Kibaha, mkoani Pwani
jana. Kushoto ni Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven.
Mkuu
wa Wilaya ya Kibaha, mkoani Pwani, Mheshimiwa Asumpter Mshama wa pili
kutoka kulia, akiwa kwenye picha ya pamoja na mshindi wa Biko wa Sh
Milioni 20 aliyepatikana katika droo ya 19, mkazi wa Mlandizi, Elisiana
Laizer kulia kwake mwenye gauni jekundu. Kushoto ni Meneja Masoko wa
Biko Goodhope Heaven na mmoja wa watendaji wa juu wa benki ya NMB kwenye
tawi la Mlandizi.
“Nimeshuhudia kwa macho yangu umekabidhiwa fedha hizi Sh
Milioni 20 kutoka kwa watu wa Biko, hivyo nitaanza kukufuatilia hatua kwa hatua
ukizingatia kuwa upo katika wilaya yangu na mimi kama DC nimekuja hapa
kushirikiana na wananchi ili tupige hatua kiuchumi,” Alisema DC Mshama.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa fedha zake, Elisiana Laizer
alisema mbali na kuwa ni mjasiriamali wa kuuza sabuni, lakini hatakuwa na
papara katika matumizi ya fedha zake alizokabidhiwa baada ya kushinda Biko droo
ya 19, huku akiwa ni mchezaji mzuri wa mchezo huo.
“Nashukuru kwa kupewa fedha hizi lakini kwakuwa ni nyingi
sana, nitatuliza akili yangu badala ya kufanya papara katika kuzitumia, maana
ndoto yangu ni kuhakikisha kuwa fedha zinakuza uchumi wangu, hivyo nawashauri
Watanzania wenzangu tucheze Biko ili tuweze kuibuka na ushindi wa droo kubwa ya
Sh Milioni 20 ya Jumatano na Jumapili,” Alisema.
Naye Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, aliwataka
Watanzania kuendelea kuchangamkia mchezo wao ili waweze kuvuna donge nono la
Jumatano na Jumapili pamoja na kuzoa zawadi za papo kwa hapo zinazoanzia Sh
5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja, huku namba
ya kampuni ni 505050 na ile ya kumbukumbu ni 2456, huku gharama ya mchezo
ikianzia Sh 1000 na kuendelea na ukichezwa kwa kutumia simu za M-Pesa, Tigo
Pesa na Airtel Money.
“Leo tumemkabidhi mshindi wetu wa Mlandizi sambamba na kupewa
elimu ya kifedha kutoka kwa wataalam wa benki ya NMB wa tawi la Mlandizi,
wilayani Kibaha, mkoani Pwani, huku ikiwa Biko imeendelea kutoa ushindi kwa
wachezaji wetu wa mikoa mbalimbali ya Tanzania, hivyo tunaomba Watanzania
wacheze kwa wingi na mara nyingi zaidi ili waweze kuibuka na mamilioni ya Biko,”
Alisema Heaven.
Kwa miezi miwili tangu kuanza kwa bahati nasibu ya
Biko, Biko
imetoa zaidi ya Sh Bilioni moja kwa washindi katika miezi miwili ya Mei na
Juni, ikiwa ni njia ya kuwanufaisha wachezaji wao hapa nchini.
SHARE
No comments:
Post a Comment