Tume
ya Vyuo Vikuu Tanzania ( TCU) umeutangazia Umma kuwa kuanzia Julai 22
mwaka huu vyuo vyote vya elimu ya juu hapa nchini vitaanza kupokea
maombi ya udahili kwa mwaka wa masomo 2017/2018.
Kaimu
Katibu Mtendaji wa Tume hiyo Prof. Eleuther Mwageni ameyasema hayo
jana, Jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu
ya kuanza rasmi udahili kwa mwaka 2017/2018.
Prof.
Mwageni alisema kuwa waombaji wanatakiwa kutuma maombi yao kwenye vyuo
husika na siyo tena TCU kama ilivyokuwa kwa mwaka jana na miaka mingine
ya nyuma.
Aidha
alisema kuwa waombaji wahakikishe wanaomba programu za masomo ambazo
zimeidhinishwa na kutambuliwa na TCU na Baraza la Taifa la Elimu ya
Ufundi (NACTE).
“Tunavikumbusha
vyuo kutangaza programu ambazo zimeidhinishwa na kutambuliwa na TCU na
NACTE, ikiwa chuo kitatangaza programu ambazo hazitambuliki na Tume,
basi chuo husika kitachukuliwa hatua,” alisema Prof. Mwageni.
Aliendelea
kwa kusema kuwa, orodha ya programu hizo inapatikana katika tovuti ya
TCU ( www.tcu.go.tz) ambapo programu hizo zimegawanywa katika makundi
mawili yaani Kidato cha Sita na Diploma.
Vile
vile, Prof. Mwageni aliwataka waombaji watakao chaguliwa kwa zaidi ya
chuo kimoja, kuthibitisha kwa wakati chuo watakachokwenda ili kutoa
nafasi kwa waombaji wengine.
Waombaji wamehimizwa kusoma kwa makini mwongozo wa udahili kwa mwaka 2017/18 ambao unapatikana kwenye tovuti ya Tume.
Aidha
Tume inawakaribisha wadau wote kushiriki maonesho ya Elimu ya Juu,
Sayansi na Teknolojia yatakayofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja, Jijini
Dar es Salaam kuanzia Jula 26 hadi 29 mwaka huu ambapo zaidi ya vyuo 80
vinatarajiwa kuwepo katika maonesho hayo.
Na: Lilian Lundo – MAELEZO.
SHARE
No comments:
Post a Comment