WABUNGE NANE CUF WATINGA MAHAKAMANI KUPINA KUVULIWA UBUNGE, MTATIRO AIBUKA
Wakati wabunge nane wa CUF waliovuliwa uanachama na kuvuliwa ubunge wao
wametinga leo mahaka ya Kisutu kupinga kuvuliwa ubunge wao, Mwenyekiti
wa kamati ya uongozi wa chama cha Cuf anayetambuliwa na upande wa katibu
mkuu wa Cuf Maalim Seif Sharif Hamadi ndugu Julius Mtatiro amelaani
kitendo cha spika wa bunge Job Ndugai kubariki kufukuzwa uwanachama
wabunge 8 wa viti maalum wa chama cha wananchi Cuf baada ya kile
kilichoitwa kutokutii wito wa uongozi wa chama hicho unaotambuliwa na
msajili wa vyama
Mtatiro alisema hayo jana baada ya ofisi ya spika kutoa taarifa kwa
uma juu ya hatua ambazo zimechukuliwa na uongozi wa chama cha Cuf chini
ya mwenyekiti wake anayetambuliwa na msajili wa vyama vya siasa, Prof
Ibrahimu Lipumba.
Wakati wabunge nane wa CUF waliovuliwa uanachama na kuvuliwa ubunge wao
wametinga leo mahaka ya Kisutu kupinga kuvuliwa ubunge wao, Mwenyekiti
wa kamati ya uongozi wa chama cha Cuf anayetambuliwa na upande wa katibu
mkuu wa Cuf Maalim Seif Sharif Hamadi ndugu Julius Mtatiro amelaani
kitendo cha spika wa bunge Job Ndugai kubariki kufukuzwa uwanachama
wabunge 8 wa viti maalum wa chama cha wananchi Cuf baada ya kile
kilichoitwa kutokutii wito wa uongozi wa chama hicho unaotambuliwa na
msajili wa vyama.
Akieleza kwa masikitiko makubwa Mtatiro amesema Jumatatu Lipumba na
Sakaya walimuandikia Spika wa Bunge kumjulisha kuwa “Baraza Kuu la CUF”
limewafukuza uanachama Wabunge 8 wa Viti Maalum wa CUF kitu ambacho ni
kinyume na taratibu za chama cha Cuf kwa sababu katibu mkuu wa Cuf
Maalim Seif alishamwandikia Spika Ndugai kumjulisha kuwa baraza kuu
halali la cuf ni lile lililochaguliwa mwaka 2014 kwenye mkutano mkuu wa
chama cha wananchi Cuf.
Jumanne ya wiki hii Ofisi ya Bunge ilitoa taarifa kwa umma kuujulisha
kuwa imepokea maelekezo kutoka kwa Sakaya na Lipumba kuwa wabunge hao 8
si wanachama na Ofisi hiyo ikaeleza kuwa bado inatafakari hatua za
mwisho za kuchukua, Jana Jumatano, Ofisi ya Bunge imetangaza uamuzi
wake, kwamba inakubaliana na uamuzi wa Cuf ya Lipumba na Sakaya na kuwa
imewavua wabunge hao 8 ubunge wao wa Viti Maalum, na kuwa imeiandikia
Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuijulisha kujaza nafasi hizo zilizo wazi.
“Nataka kuwaeleza wanachama na watanzania wote, kwamba viongozi wa chama
wanakutana kuendelea kuchukua hatua. Tunajua kuwa vyombo vya Serikali
hivi sasa vinafanya kazi kubwa kuhakikisha kuwa aidha CUF inamkubali
“MSALITI” Lipumba kuwa Mwenyekiti wake, au CUF isambaratike. Na
suluhisho la hali hii haliwezi kuwa kukaa chini na MSALITI.”alisema
Julius Mtatiro
Mtatiro amewatahadharisha wanachama wenzake kuwa wanapopambana na
wasaliti waliokubuhu na wako ndani ya nyumba yao, vita yake siyo ndogo
lakini amewataka wasimame imara kwa sababu anaamimi kuwa CUF itavuka
misukosuko hii.
Kwa jicho moja wapo watu wanachekelea na kudhani kadhia hii ni ya CUF
tu, mimi natizama hali hii kama Mapambano ya Dola ya kuhakikisha vyama
mbadala vinaongozwa na wasaliti ili Dola iendelee kuwatumia kuzamisha
demokrasia ushindani wa kisiasa nchini,amesisitiza Mtatiro ambaye kwa
sasa yuko nchini masomoni nchini Marekani.
Mtatiro amesema dola ikifanikiwa kuisambaratisha CUF, vyama vingine vya
upinzani havitakuwa salama, taasisi zingine za kiraia hazitakuwa salama
pia. Mtatiro ameongeza kuwa mtu anayeyatizama mapambano haya kama vita
ya ndani ya CUF hajaisoma dunia . Haya ni mapambano makubwa, dhidi ya
demokrasia ya Tanzania,amesisitiza Mtatiro
Mtatiro amesema yeye ni mwanademokrasia imara na hatayumbishwa na
Wasaliti.
Mtatiro amesema Cuf kumkubali Lipumba na genge lake itakuwa na
maana ya kuiua Cuf moja kwa moja Tanzania Bara, maana alipojaribu
kukimbia mwaka 2015, ndipo Cuf iliibuka na kuwa chama imara mara 10
Tanzania bara,na kurudishwa kwake kwa nguvu kunakofanywa na dola ni
mkakati wa kuimaliza Cuf na suluhisho lake haliwezi kuwa Cuf kumtambua
Lipumba.
Mtatiro ameweka wazi kuwa hata dola ikifanya nini, Lipumba ameshadharaulika na hawezi kuisaidia tena dola hii yenye upofu.
SHARE
No comments:
Post a Comment