Moja ya taarifa niliyoipokea kutoka Arusha
ni kuhusu Wafanyabiashara wadogo wadogo wanne wa Madini akiwemo Makamu
Mwenyekiti wa wafanyabiashara hao, Ngalae Mapera kudaiwa kumwagiwa
tindikali usoni na watu wasiofahamika.
Tukio
hilo limetokea katika eneo la St Thomas, Arusha ambako watu
wasiofahamika walifika katika eneo hilo wakiwa kwenye gari aina ya Rav 4
ya rangi ya Blue na waliposhuka waliwamwagia maji yanayosadikiwa kuwa
na kemikali
Mmoja
wa mashuhuda wa tukio hilo Ole Laiser alisema baada ya gari kusimama
walishuka wanawake wanne ambao hawakujulikana na kuwafuata
wafanyabiashara hao kisha kuanza kubishana kuhusiana na masuala ya
fedha.
"Sisi
tuliona baada ya wao kufika hapa waliegesha gari lao na kuwafuata
wenzetu ambapo walikuwa wakibishana sana. Baada ya muda tulimuona mmoja
wa wanawake akirudi kwenye gari tukajua ameenda kufuata bastola na baada
ya muda alikuja ameshika chupa na kuwamwagia wenzetu.” – Ole Laiser.
Wafanyabiashara waliofikwa na tukio hilo ni Lucas Kiruswa, Sebastian Laiser, Moringe Issa pamoja na Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wadogo wa Madini Ngalae Mapera.
Kamanda
wa Polisi Arusha, Charles Mkumbo amethibitisha kutokea tukio hilo na
kusema Polisi wangali wanachunguza undani wa tukio hilo na watatoa
taarifa kamili baada ya uchunguzi kukamilika.
SHARE
No comments:
Post a Comment