Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
ROBO
fainali ya Ndondo Cup inaendelea tena siku ya Alhamisi kwa timu nane
kuumana katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo Uwanja wa Kinesi.
Droo hiyo
iliyochezeshwa jana na kila timu kufahamu anapambana na nani katika
hatua ya robo iliweza kuwa ya aina yake baada ya watangazaji wa vipindi
mbalimbali wa Clouds kugawana timu hizo na kuwapa ahadi lukuki .
Hii ndo Ratiba ya Robo fainali
Alhamis 27/07/2017
Vijana Rangers vs Kibada one
Ijumaa Tar 28/07/2017
Goms United vs Mlalakuwa Rangers
Jumamosi Tar 29/07/2017
Mpakani Combine vs Misosi Fc
Jumapili Tar 30/07/2017
Keko Fanicha vs Stimutosha Fc
Leo tena
wenyewe wamebaki na timu yao Mlalakuwa Rangers, kwa hiyo hawakuwepo
kwenye draw ya kila kipindi kupata timu yake. XXL wao timu yao ni Keko
Furniture, Jahazi wenyewe wameangukia kwa Mpakani Kombaini, Clouds 360
timu yao ni Misosi FC wakati amplifier watakuwa na Vijana Rangers,
Kibada One wameangukia kwa Power Breakfast huku Goms United wakitua kwa
Shilawadu na Stim Tosha ikienda kwa wazee wa Alasiri.
Baada ya
droo hiyo kila kipindi kilitoa ahadi na mbwembwe kibao na kuziahidi timu
hizo kuwa watanunua kila goli huku kipindi cha 360 wakitoa ahadi ya
kuwapeleka mbuga za wanyama iwapo watakuwa mabingwa.
SHARE
No comments:
Post a Comment