Wizara ya utumishi
wa umma nchini Uganda imewafahamisha wafanyakazi wa serikali kuvalia
nadhifu na kuwaonya wanawake dhidi ya kuonyesha vifua vyao.
Wanawake wanaruhusiwa kuvalia suti za long'i, lakini wale walio wafanyakazi wa serikali hawaruhusiwi kuvalia mavazi ya kuwabana.
Ilani hiyo inasema kuwa mavazi ya urembo yanastahili kuwa nadhifu na wanawake hawaruhusiwi kupaka nywele zao rangi inayong'aa au kuwa na nywele ya kuongezwa.
Wanaume nao watakiwa kuvalia nadhifu, shati za mikono mirefu, koti na tai, wasivae suruali za kubana, wawe na nywele fupi na safi na wasivae mavazi ya rangi zinazong'aa.
Hata hivyo masharti hayo hayajaonekana kuanza kufuatwa hadi sasa.
SHARE
No comments:
Post a Comment