WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri
ya wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, Bw. Eliseyi Mgoyi pamoja na maofisa
wengine watatu kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za umma.
Pia
amemuagiza Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(TAKUKURU) mkoa wa Songwe, Damian Sutta kuwakamata na kuanza
kuwachunguza haraka maofisa hao na kisha ampelekee taarifa ofisini
kwake.
Waziri
Mkuu amewasimamisha kazi maofisa hao Jumapili, Julai 23, 2017
wakati alipozungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi
kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari Vwawa, akiwa katika ziara ya mkoa wa
Songwe.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Watumishi wa Umma, Viongozi wa
Dini na Viongozi wa Taasisi Binafsi wa wilaya ya Mbozi kwenye ukumbi wa
Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Vwawa wilayani Mbozi Julai 23, 2017.
Kulia ni mkewe Mary na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa
Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Limdi, Erasto Zambi
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa jengo la Mkuu wa Mkoa wa
Songwe nje kidogo ya mji wa Vwawa mkoani Songwe Julai 23, 2017. Kushoto
ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (kulia kwake) wakitazama Kimondo
wakati walipotembelea Kituo cha Mambo ya Kale cha Mbozi mkoani Songwe
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakiwapungia wananchi wa wilaya ya
Mbozi wakati walipowasili kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari ya Kyalele
wilayani humo kuhutubia mkutano wa hadhara, Julai 23, 2017. Kulia ni
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakitazama nguo za batiki wakati
walipotembelea banda la wanawake wajasiriamali wa Mbozi kabla ya
mkutano wa hadahara uliohutubia wa Waziri Mkuu kwenye uwanja wa Shule
ya Sekondari ya Nalyelye wilayani Mbozi, Julai 23, 2017. Kulia ni
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
SHARE
No comments:
Post a Comment