Baba
Mzazi wa Msanii Diamond Platinum, Abdul Naseeb amefunguka kuhusu tetesi
zinazoendelea za mtoto wake kutajwa kuwa ndiye mzazi halali wa mtoto wa
mlimbwende Hamisa Mobeto anayetambulika kwa jina la Abdul Naseeb ambalo
ndiyo jina la baba yake na Diamond.
Akizungumza katika kipindi cha SHILAWADU cha Clouds TV Ijumaa hii, Baba
Diamond ameeleza kuwa kama Diamond ameamua kumpa mtoto huyo jina lake ni
upendo na inaonesha thamani kwake.
Baba Diamond amesema hawezi kumlaumu mwanaye Diamond kwa kilichotokea
kwani yeye ni msanii mkubwa anakumbana na vishawishi mbalimbali, hivyo
cha kufanya asiendekeze zinaa awaoe wanawake aliozaa nao (Hamisa Mobeto
na Zarina Hassan) na awatendee haki kwa kutoa huduma sawa.
Kuhusu wajuukuu zake, Mzee Abdul ameeleza kuwa yeye anawapenda wote ingawa hajawahi kumuona hata mmoja.
Alhamisi hii Diamond aliandika maneno makali mtandaoni yaliyohusishwa
kwenda Mobetto ambaye siku chache zilizopita alitangaza jina mwanaye
kuwa Abdul Naseeb. Hatua hiyo iliwafanya mashabiki wengi ambao walitaka
kumjua baba wa mtoto huyo wa Mobetto kuwa ni Diamond.
Hata hivyo mpaka sasa mkali huyo wa wimbo Eneka hajawahi kutoa neno
lolote juu ya mtoto huyo licha ya mama yake pamoja na dada yake Esma
kuonekana mara kadhaa wakimtembelea mrembo huyo wakati alipojifungua
katika hospitali moja jijiji Dar es salaam.
SHARE
No comments:
Post a Comment